Home SPORTS SIMBA SC YAMALIZA MWENDO KIBABE HATUA YA MAKUNDI SHIRIKISHO

SIMBA SC YAMALIZA MWENDO KIBABE HATUA YA MAKUNDI SHIRIKISHO

Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC imefuzu hatua ya robo fainali kwa kishindo baada ya kuichapa timu ya CS Constantine mabao 2-0 katika mchezo wao wa kundi A, uliopigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Da es Salaam.
Ushindi huo wa Simba unaifanya timu hiyo kuongoza kundi  A na kushika nafasi ya kwanza ikiwa na alama 13 dhidi ya wapinzani wao wenye alama 12 wakiwa wameshika nafasi ya pili.

Magoli ya Simba SC yamepatikana katika kipindi cha pili cha mchezo huo likifungwa na Kibu Denis Prosper kwa mkwaju mkali uliomshinda mlinda mlango wa CS Constantine, ambapo goli la pili lilifungwa  na Leonel Ateba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here