Home LOCAL SERIKALI YAFANIKIWA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA MAGOJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE

SERIKALI YAFANIKIWA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA MAGOJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE

Serikali kupitia Wizara ya Afya imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika mapambano dhidi ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo matende na mabusha na Minyoo ya tumbo.

Alikalika Halmashauri 114 Nchini Tanzania zimefanikiwa kupunguza maambukizi chini ya asilimia mbili, hatua ambayo imepelekea kuacha kugawa kinga tiba dhidi ya ugojwa huo

Kaimu Meneja wa Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTDCP), Dk. Faraja Lyamuya, amebainisba hayo jijini Dar es salaam wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wandishi wa habari kuhusu magojwa hayo.

Dk. Lyamuya ameeleza kuwa licha ya mafanikio hayo, changamoto bado ipo kutokana na imani potofu zinazosababisha baadhi ya jamii kusita kushiriki katika kampeni za mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Ameongeza kuws baadhi ya watu wanaamini kuwa matende na mabusha ni magonjwa ya kurithi, yanaweza kusababishwa na kulogwa, au ni magonjwa yanayoathiri maeneo ya Pwani pekee

Nae Afisa Mpango wa NTDCP, Dk. Lilian Ryatura, amesema kuwa halmashauri 69 zilizokuwa na maambukizi makubwa ya ugonjwa wa Trachoma (vikope), baada ya utoaji wa kingatiba ya Zithromax, idadi hiyo imepungua hadi halmashauri tisa tu.

Amesisitiza kuwa ugonjwa huo unahitaji upasuaji mdogo wa kusawazisha kope ili kupona.

Dkt. Mohamed Nyati, Afisa Mpango wa NTDCP, amewakumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kumeza kingatiba za Kichocho kila zinapotolewa, huku akisisitiza kuwa ugonjwa huu unaweza kuepukika kwa kuepuka maeneo yenye maji yaliyotuama.

Hata hivyo Afisa Mpango mwingine, Ruth Mchomvu, ameeleza kuwa zaidi ya watu milioni 7.2 wanaishi katika mikoa ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Songwe, Tanga, Iringa, Njombe, Iringa na Dodoma, ambapo wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa Usubi, ambao unaweza kutibika kwa urahisi.

Kwa upande wake Afisa Mpango Catherine Mahimbo ameeleza madhara ya ugonjwa wa minyoo ya tumbo, ikiwa ni pamoja na utapiamlo, kupungua uzito, na madhara makubwa kwa watoto, kama vile udumavu wa akili na mwili.

Aidha Mafunzo haya ya siku moja, yaliyoandaliwa na NTDCP, ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Duniani, ambayo hufanyika kila tarehe 30 Januari, na kauli mbiu ya mwaka huu 2025 ni “Tuungane. Tuchuke hatua. Tutokomeze Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here