Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mwaka 2025 CCM wana jambo lao la kuhakikisha wanazima zote na kuwasha kijani na kukifanya Chama cha Mapinduzi kiibuke Mshindi kwenye Uchaguzi.
Akihutubia kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Jijini Dodoma leo January 18,2025, Rais Samia amesema “Nawatakia tena kheri ya mwaka mpya 2025, mwaka ambao ni wetu kwani mwaka huu tuna jambo letu, kama wanavyosema Vijana wetu wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ni mwaka wa kuzima zote na kuwasha kijani”
“Nimeambowa leo kuna mpira tumalize mapema, kama mnavyofahamu CCM iliridhia ombi la Kinana kupumzika kwa muktadha huo nafasi hiyo ipo wazi, tunamshukuru Kinana na kumpongeza kwa Uongozi wake thabiti na kumuhakikishi ushirikiano wetu”