Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu. Stephen Wasira akizungumza kwa kutoa shukrani kwa kuaminiwa na kuchaguliwa katika nafasi hiyo mbele ya Viongozi na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaifanyika katika ukumbi wa JKCC Jijini Dodoma.
“Kazi yetu ya kwanza ni kushika dola kwa serikali zote Tanzania Bara na Zanzibar, sasa katika serikali za mitaa tayari na tumefanya vizuri sasa kazi tuliyonayo ni kukamata dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar”
“Tujiandae vema na ikifika mwezi Oktoba tutakamata dola kwa kura nyingi za ushindi na kura unazipata kwa kutekeleza ahadi na ilani ya chama chako, sisi CCM tumetekeleza kwa kishindo chini ya Mwenyekiti na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan”
“CCM hatuna sababu ya kushindwa uchaguzi, Miradi yote inatekelezwa kwa wakati na maendeleo yanafanyika”
“Twendeni tukashinde uchaguzi, sababu tunazo, nia ipo na uwezo tunao, huu ndio wito wangu na kazi inaanza”
“Nataka Dunia ijue , wana CCM na wasio wana CCM, Chama chetu ni cha umoja, amani na maendeleo, tunapewa nchi ili kufanya kazi na haiwezi kufanyika kama hakuna amani, Mwenyekiti wetu ana falsafa ya 4R na mimi nasema kazi nitakayoanza nayo ni kuendeleza maridhiano na wengine wanasema hakuna maridhiano, hapana haturidhiani na mtu mmoja bali tuna ridhiana na jamii yenye wadau wengi na viongozi wa kidini, tutasaidiana nao katika maridhiano kwasababu CCM ni chama cha amani, kama una chama chako kinataka vita sisi tutazungumza na wewe kuwa huko hatuendi kwakuwa amani ni msingi wa maendeleo”
#MkutanoMkuuCCM2025
#CCMImara
#VitendoVinaSauti
#KaziIendelee