Home LOCAL MIGOGORO YA ARDHI KINARA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA

MIGOGORO YA ARDHI KINARA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA

Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro,akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Januari 20,2025 Mtumba jijini Dodoma kuelekea uzinduzi wa kampeni ya  Msaada wa Kisheria ya Mama Samia itakayofanyika katika mikoa 6 ya ambayo ni Kigoma, Katavi, Geita, Kilimanjaro, Tabora na Mtwara.

Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro,akizungumza na waandishi wa habari  leo Januari 20,2025 Mtumba jijini Dodoma kuelekea uzinduzi wa kampeni ya  Msaada wa Kisheria ya Mama Samia itakayofanyika katika mikoa 6 ya ambayo ni Kigoma, Katavi, Geita, Kilimanjaro, Tabora na Mtwara.

Katibu Mkuu Wizara ya  Katiba na Sheria Bw.Eliakim Maswi,akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 20,2025 Mtumba jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro amesema tangu kuanza kwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN) na kupita katika mikoa 11 nchini , eneo la ardhi limeonekana kuwa na migogoro mingi inayopelekea kwenda kwenye jinai.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 20,2025 Mtumba jijini Dodoma kuelekea uzinduzi wa kampeni hiyo itakayofanyika katika mikoa 6 ya ambayo ni Kigoma, Katavi, Geita, Kilimanjaro, Tabora na Mtwara.

Dkt. Ndumbaro amesema mpaka sasa Kampeni hiyo imeshawafikia Watanzania takribani 775,119 wakiwemo Wanawake 380,375 na Wanaume 394,744 ambapo jumla ya Migogoro 693 imetatuliwa na kuhitimishwa kati ya migogoro 3,162 iliyopokelewa katika Mikoa 11 iliyofikiwa na Kampeni.

“Kampeni ya Msaada wa Kisheria ni mkombozi mkubwa kwa Wananchi Wanyonge na wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za Mawakili na mfumo mzima wa Sheria.Kupitia Kampeni hii Wanyonge wanasaidiwa kupunguza malalamiko katika sekta ya Sheria kwa kusimamia kikamilifu Sheria ya Utoaji Haki,”amesema.

Ameongeza kuwa kupitia kampeini hiyo wanatimiza Ilani ya CCM ambayo imefafanua kwa kina kila sekta jambo la kufanya na katika sekta yao ya utoaji haki imebainisha itakavyohakikisha wananchi wanapata haki kwa gharama nafuu na kwa wakati, wananpata elimu ya kisheria hivyo wao wanatekeleza ilani na kuwakumbusha kuwa Serikali imara haiishii kutekeleza hilo pekee. bali inaenda kulitengenezea nyaraka na muongozo wa kulitekeleza vyema.

Amesema migogoro ambayo imetataliwa mpaka sasa kupitia kampeni hiyo imesaidia kuokoa muda wa kutosha kwa wananchi na rasilimali fedha ambavyo kwaasasa wanavitumia kwenye kuleta maendeleo na kuzalisha zaidi na migogoro itakuwa imekwisha.

“Mpango huu ni mkombozi kwa wanyonge wasio kuwa na uwezo wa kumudu gharama za mawakili, kumudu mfumo mzima wa sheria kwasababu unakuta mwingine hata kulipia nyaraka moja ya sheria hawezi kwahiyo huu ni mkombozi pia inamsaidia mnyonge kupunguza malalamiko katika sekta ya sheria na utoaji haki kwasababu kulalamika nako ni kadhia,”amesema.

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ilizinduliwa rasmi Februari 15, 2023 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Dkt. Damas Ndumbaro ambapo inatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia Machi 2023 hadi Februari 2026, katika mikoa yote ta Tanzania Bara na Visiwani ikiwa mpaka sasa imepita katika mikoa 11.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here