Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amesema maandalizi ya kusherehekea siku ya mfanano wa tarehe ya kuzaliwa rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ifikapo tarehe 27 Januari 2025
Akizungumza na wanahabari mapema leo, Januari, 22 ,2025 amesema kuwa wamejipanga kusherehekea ‘birthday” ya Rais hodari na mchapakazi na kutawa na tutakata keki na kusherehekea pamoja na wananchi wa Kisarawe huku wakimuimbea dua njema kwa Mwenyezi Mungu azidi kumpa afya na umri ili aweze kulitumia taifa lake.
“Tuna Rais hodari, shupavu,na mchapakazi hivyo basi sisi Wanakisare tutasherehekea siku hiyo kwa kukata keki na tutakula kwa pamoja,hivyo nawakaribisha Wananchi wote wa Kisarawe, amesema Magoti
Aidha DC Magoti amesema kuwa Januari 25 asubuhi kutafanyika uzinduzi wa wiki ya sheria utakaofanyika kwenye uwanja wa Chanzige Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani ambapo huduma ya kisheria itaendeshwa kwa juma moja huku kilele chake kitafanyika Februari mosi .
Huduma za Kimahakama zitafanyika kwenye Kata zote za Kisarawe wananchi ambao wanakabiliana na migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa na mengineyo wameombwa kujitokeza kupata huduma hiyo.ambayo itaanza saa moja asubuhi hadi jioni
Pia DC Magoti ametoa onyo kali kwa wazazi hawawapeleki watoto shuleni bila ya kuwa na sababu maalumu kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Naye Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisarawe Mhe.Emmy Amon Nsangalufu amesema kuwa wiki ya sheria itatolewa tarehe 25 hadi 31 Januari mwaka huu pia kutakuwa na gari ambalo litakuwa mfano wa Mahakama inayotembea huku lengo likiwa kuwafikia wananchi na kuwapa huduma wanayostahili.
Nsangalufu ametoa wito kwa wananchi kuwa Mahakama ni mali ya wananchi hivyo waitumie kwa manufaa yao na siku ya uzinduzi wataanza na maandamano asubuhi kwenda kukutana Uwanja wa Chanzige.
” Tumejipanga kuwafikia wazee na watu wote wasiojiweza ndani ya kata zote 17 tutakuwa na gari pamoja na Mawakili wabobevu katika kutatua shida zao” amesema Nsangalufu.