Home LOCAL DOROTH SEMU ATANGAZA KUWANIA URAIS

DOROTH SEMU ATANGAZA KUWANIA URAIS

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu ametangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao.

Semu ametangaza nia hiyo leo Alhamisi Januari 16, 2025 alipokuwa akizungumza na wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akisisitiza yupo tayari kumkabili Rais Samia Suluhu Hassan wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Ndugu zangu, Tanzania inahitaji uongozi mpya utakaolinda masilahi ya Taifa na uchumi imara, jamii yenye fursa sawa, na uongozi wa uwazi. Tunaweza kubadilisha hali hii kwa kushirikiana, kuondoa changamoto hizi, na kuimarisha mustakabali wa Taifa letu.