• Faida Kabla ya Kodi: TZS bilioni 931, ongezeko la 20% kwa mwaka
Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!• Faida Baada ya Kodi: TZS bilioni 644, ongezeko la 18% kwa mwaka
• Jumla ya Mapato: TZS trilioni 1.64, ongezeko la 16% kwa mwaka
• Jumla ya Mali: TZS trilioni 13.7, ongezeko la 13% kwa mwaka
• Uwiano wa mapato na matumizi (CIR): 38%
Dar es Salaam, Januari 31, 2025,
Mwaka 2024, Benki ya NMB iliendeleza kasi ya ukuaji, ikipata matokeo ya kipekee ya kifedha na kiutendaji, yaliyochochewa na ukuaji imara wa mizania, ufanisi wa uendeshaji, na umakini mkubwa katika ukopeshaj
Benki ya NMB ilipata faida kubwa ya kabla ya kodi kuwahi kupatikana katika historia yake kwa kufikia TZS bilioni 931 ambao ni ukuaji wa kasi wa 20% ikilinganishwa na TZS bilioni 775 za mwaka wa fedha 2023. Hii ilipelekea kupatikana kwa uwiano wa Faida na Mtaji wa 28%.Ukuaji huu imara wa faida ulitokana na ongezeko la mapato, ufanisi mkubwa wa uendeshaji, na mwendelezo wa kuimarisha ubora wa mkopo. Jumla ya mapato iliongezeka kwa 16% hadi TZS trilioni 1.6, kutokana na ongezeko la Mapato ya Riba Halisi kwa 13% na Mapato Yasiyo ya Riba kwa 23%.
Uwiano wa mapato na matumizi (CIR) uliimarika kwa pointi za asilimia 100 hadi 38%, ambao ni chini ya ukomo wa kikanuni wa 55%. Maboresho haya yalichangiwa na ufanisi zaidi wa uendeshaji, usimamizi makini wa matumizi, na uwekezaji wa kimkakati kuendeleza rasilimali watu na katika teknolojia za kidijitali. Hii iliiwezesha benki kuendeleza ukuaji, na kuhakikisha ufanisi na thamani vinapatikana katika shughuli zake zakifedha za msingi. Juhudi zote hizi zinathibitisha uwezo wa Benki ya NMB katika kupata uwiano mzuri kati ya ufanisi na ubunifu, huku ikijenga msingi imara wa mafanikio ya baadaye.
Aidha, Mizania ya Benki iliendelea kukua, huku jumla ya mali ikiongezeka kwa 13% kwa mwaka mzima wa 2024 hadi TZS trilioni 13.7. Mikopo halisi kwa wateja ilikua kwa 10% hadi TZS trilioni 8.5, huku amana zikiongezeka kwa 13% hadi TZS trilioni 9.5. Ukuaji huu thabiti unaakisi dhamira ya NMB katika kuendeleza ujumuishaji wa kifedha, ambao umesaidia kuongeza idadi ya wateja wapya na kiwango cha mikopo, kuboresha huduma kwa wateja na imani yao kwetu, huku tukindelea kuja na masuluhisho mapya bunifu na rahisi ya kifedha.
Benki pia iliendelea kuimarisha ubora wa mikopo, ambapo uwiano wa mikopo chechefu (NPL) ulipungua hadi 2.9% mwaka 2024 kutoka 3.2% mwaka 2023. Mafanikio haya yalitokana na usimamizi makini wa ukopeshaji na ufuatiliaji wa karibu wa mikopo.
NMB iliendelea pia kuwa na mtaji imara, kutokana na ukuaji wa mapato na ufanisi wa matumizi ya mtaji, hali iliyoiweka benki katika nafasi imara kifedha. Kufikia mwishoni mwa Desemba, Uwiano wa Ufanisi wa Mtaji ulikuwa 23%, kiwango ambacho ni zaidi ya uwiano hitajika kikanuni. Hii inatuweka katika nafasi nzuri ya kuongeza uwekezaji, kuzidisha mikopo, na kuendelea kuwa imara kwa muda mrefu.
Ufanisi wa utekelezaji wa mkakati wa Benki ya NMB umekuwa chanzo cha matokeo haya makubwa na ya kihistoria, na umewezesha kupigwa kwa hatua hizi muhimu katika hsitoria yetu;
NMB ni benki inayotengeneza faida kubwa kuliko benki zote Tanzania na imeweka historia ya kuwa benki ya kwanza nchini kufikia thamani ya zaidi ya dola bilioni moja. Mafanikio haya yanathibitisha hadhi ya NMB kama benki kubwa zaidi iliyoorodheshwa katika soko la hisa nchini, benki ya pili kwa ukubwa Afrika Mashariki, na kampuni ya sita kwa ujumla kwa ukubwa wa kimtaji katika soko la hisa. Utendaji thabiti wa kifedha wa NMB unaifanya kuwa miongoni mwa kampuni 30 zenye thamani kubwa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA) – bila kujumuisha Afrika Kusini, Hiyo ni kwa mujibu wa Capital Market Union (CMU) katika ripoti yake kuhusu kampuni zinazoongoza kwenye nchi za SSA.
H inaimarisha nafasi ya NMB kama kinara wa soko, ikiongoza kwa kutoa robo ya mikopo yote ya sekta ya benki nchini na kuwa na robo ya amana zake zote. Kufikia Desemba 2024, benki iliongeza wateja wapya milioni 1.5, na kufanya jumla ya wateja wake kuzidi milioni 8.6.
Benki ya NMB imethibitsiha pia dhamira yake ya ubunifu na uendelevu. Mwaka 2024, benki iliorodhesha kwa mara ya kwanza hati fungani endelevu ya NMB Jamii Bond, ambayo ni ya kwanza ya aina hiyo Kusini mwa Jangwa la Sahara, katika Soko la Hisa la London (London Stock Exchange) na Soko la Hisa la Luxembourg (Luxembourg Stock Exchange). Katika muktadha huo, NMB iliwekeza zaidi ya TZS bilioni 5.4 katika sekta za elimu, afya, na miradi inayohusiana na mabadiliko ya tabianchi, ikiimarisha dhamira yake ya kuchangia ustawi wa jamii na kuhifadhi mazingira.
Mafanikio haya yanaonesha umakini wa benki katika ufanisi wa utekelezaji wa mikakati wa utendaji wake, ukuaji, ubunifu, na uendelevu, na kuthibitisha nafasi yake kama kiongozi katika sekta ya benki kwenye ukanda huu.
Akizungumzia matokeo na ufanisi huu, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna, alisema: “Mwaka 2024 umekuwa wa kipekee kwa Benki ya NMB, ukiwa wa mafanikio makubwa ya kifedha na utendaji, ukuaji wa kimkakati, na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Matokeo haya yanaonyesha uimara wa tulivyojipanga kibiashara, kujitolea kwa wafanyakazi wetu, na uaminifu wa wateja wetu.
Katika siku zijazo, tutaendelea kuhamasisha na kukuza ubunifu, kupanua huduma jumuishi za kifedha, na kutoa thamani endelevu kwa wadau wetu wote.
Benki ya NMB imejipanga vizuri kuendeleza mafanikio yake haya mwaka 2025, ikiwa na mkakati thabiti unaolenga ukuaji, ubunifu, na uendelevu. Benki itaendelea kuwekeza katika teknolojia, vipaji, na masuluhisho yanayomlenga mteja ili kuendeleza ujumuishi wa kifedha na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Tanzania. NMB itaendeleza dhamira yake ya kudumisha uwezo wake mkubwa kifedha, kuwapa thamani wanahisa wake, na kuchangia ustawi na maendeleo ya jamii inazohudumia.