Home LOCAL CCM YAKEMEA MAKADA WANAOFANYA KAMPENI KABLA YA WAKATI SAHIHI

CCM YAKEMEA MAKADA WANAOFANYA KAMPENI KABLA YA WAKATI SAHIHI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekemea na kutoa onyo kali kwa Viongozi na Makada wa CCM kuacha kufanya kampeni za mapema za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Ubunge na kusema kuwa CCM ushahidi wa picha za wanaofanya hivyo.

Mwenyekiti Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akizungumza na Wajumbe kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Jijini Dodoma unaofanyika leo tarehe 18 na kuendelea kesho tarehe 19,2025.

β€œMasuala ya kampeni za mapema nawaasa wale wanaojipanga kwenda kugombea, masuala ya kampeni za mapema tunayakemea, tayari tumeshapata malalamiko na ushahidi wa picha za Watu wanaofanya misafara kwenda Majimboni, Watu wanaoitisha mikutano mikuu ya Majimbo kwa kisingizio cha ufugaji au mambo mengine lakini dhamira ni kujitambulisha kwa Wanachama”

β€œTuna ushahidi wa picha nyingi sana, sasa tunaomba tutoe onyo mapema, pia Viongozi na Watendaji Chama tuache kufanya kazi kwa mazoea na niwaombea Viongozi wa CCM mkasikilize Wananchi na kusikiliza kero zao”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here