Home LOCAL WAZIRI KOMBO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA DHARURA WA MAWAZIRI WA...

WAZIRI KOMBO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA DHARURA WA MAWAZIRI WA SADC ORGAN ZANZIBAR


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC- Organ), Mhe.

Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika) uliofanyika katika Afisi ya Mambo ya Nje Zanzibar tarehe 11 Desemba, 2024.

Mkutano umewakutanisha Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Nchi Wanachama wa SADC ambapo Tanzania ni Mwenyekiti wa Asasi hiyo, Malawi ni Mwenyekiti Ajaye na Zambia ni Mwenyekiti Anayemaliza Muda Wake.
Pia, Mkutano huo umejadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambayo ni pamoja na bajeti ya Misheni ya Ulinzi na usalama katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (SAMIDRC) kwa mwaka 2024 hadi 2025.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Waziri wa Ulinzi, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC- Organ), Balozi Dkt. Samweli Shelukindo, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Faraji Mnyepe, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Shaaban, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Talha Waziri pamoja na maafisa waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

http://WAZIRI KOMBO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA DHARURA WA MAWAZIRI WA SADC ORGAN ZANZIBAR

Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama Balozi, Dkt. Samwel Shelukindo.

Previous articleTANESCO TUNATHAMINI WADAU WA MAENDELEO – MHA. NYAMO-HANGA
Next articleUSHIRIKIANO WA TAIFA GAS NA WASHIRIKA WAKE KUTOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA NA MATUMIZI YA NISHATI SAFI NI UKOMBOZI KWA WANAWAKE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here