Home INTERNATIONAL WAZIRI JENISTA MHAGAMA AZUNGUMZA NA WATAALAM WA BIMA WA NHS JIJINI LONDON

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AZUNGUMZA NA WATAALAM WA BIMA WA NHS JIJINI LONDON

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akiambatana na ujumbe wake kutoka Tanzania akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bw. Ismail Rumatila, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu pamoja na wataalam wengine wamekutana na uongozi wa ‘National Health Services’ (NHS) ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kujifunza namna bora ya kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za afya kuelekea utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.

Waziri Mhagama amekutana na NHS Desemba 13, 2024 katika mji wa London nchini Uingereza ambapo pamoja na mambo mengine wameweza kujifunza namna bora ya kusimamia ubora wa huduma za afya ambapo wameonesha namna Taasisi hiyo inavyosimamia ubora wa huduma kwa wananchi wake.

Aidha, kupitia mkutano huo Serikali ya Tanzania imepata fursa ya kuanzisha ushirikiano utakaowezesha wataalam wa afya kuja kujifunza namna bora ya kuimarisha usalama wa huduma za afya, ubora na usimamizi wa huduma za afya pamoja na kujifunza utaratibu wa kusimamia mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote ambao unategemea kuanza utekelezaji wake.

Previous articleKURUDI KWA MINADA YA MADINI MIRERANI KUTASAIDIA KUONGEZA THAMANI YA MADINI – WADAU MADINI
Next articleHAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DISEMBA TAREHE 14, 2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here