Home LOCAL WAZIRI DKT. GWAJIMA ASISITIZA USHIRIKIANO WA WADAU NA SERIKALI KUPINGA UKATILI WA...

WAZIRI DKT. GWAJIMA ASISITIZA USHIRIKIANO WA WADAU NA SERIKALI KUPINGA UKATILI WA WATOTO MTANDAONI 

Na WMJJWM-Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito kwa wadau mbalimbali chini kushirikiana katika kuweka mikakati mbalimbali ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto mtandaoni.

Waziri Dkt Gwajima ameyasema hayo Desemba 17, 2024 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Usalama wa Mtoto Mtandaoni.

Waziri Dkt. Gwajima amesema umuhimu wa kuwa na Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Masuala ya Usalama wa Watoto Mtandaoni kwa lengo la kushauri Serikali namna bora ya kuwalinda watoto dhidi ya ukatili kupitia mitandao kwani masuala ya ukatili wa watoto mtandaoni ni masuala mtambuka na zaidi, yanahitaji nguvu na uratibu wa pamoja miongoni mwa Sekta za Serikali, Sekta Binafsi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. 

“Kamati hii muhimu, inajumuisha Wataalam mbalimbali kutoka kwenye Sekta mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi wa Wizara zinazohusika na masuala ya ulinzi wa watoto na wataalam waliobobea katika matumizi ya TEHAMA hapa nchini ili kutoa ushauri unaofaa katika kudhibiti ukatili wa watoto mtandaoni” amesema Waziri Dkt. Gwajima 

Aidha Waziri Dkt Gwajima amesema katika kujifunza ilikuwa na mikakati mbalimbali ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto mtandaoni Tanzania pia ilipata fursa ya kuwasilisha kazi zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na ukatili wa Watoto mtandaoni katika Mkutano wa Usalama wa Watoto Mtandaoni uliofanyika tarehe 04-05 Desemba, 2024 Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. 

Pia Waziri Dkt. Gwajima amesema katika Mkutano huo alipata fursa ya kuwa na mkutano wa pembeni na Mkurugenzi Mkuu wa WeProtect Global Allince na kumshirikisha Mkurugenzi huyo jitihada za Tanzania na vipaumbele ikiwemo hitaji la kuwa na kadi ya simu kwa ajili ya watoto (kids sim card), teknolojia ambayo inaweza kusaidia katika kupambana na ukatili wa watoto mtandaoni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku amesema Kamati hiyo iliundwa kwa lengo la kuweka mikakati mbalimbali ya kuwalinda watoto dhidi ya ukatili hasa ukatili wa mtandaoni kwani kumekuwa na changamoto kubwa ya Watoto kufanyiwa ukatili mtandaoni.

“Kamati hii ni muhimu sana kwa Ustawi wa Watoto nchini tupo hapa kuangalia masuala muhimu tuliyofanikiwa katika kupambana na changamoto hii ya ukatili wa watoto mtandaoni na kuona namna ya kuboresha zaidi ili kupunguza au kuondokana na vitendo hivi” amesema Kitiku

Nao baadhi ya Watoto kutoka Baraza la Watoto Mkoa wa Dodoma wamesema watatumia elimu ya kupambana na ukatili wa watoto mtandaoni kuwafikishia wenzao katika maeneo mbalimbali ikiwemo shuleni ili kusaidia watoto kuelewa na kujiepusha na kufanyiwa ukatili mtandaoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here