Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF, Deudatus Balile, akizungumza alipokuwa akitoa maoni yake katika Mkutano wa Wahariri na Wamiliki wa Vyombo vya Habari, kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, uliofanyika leo Disemba 16, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa JNICC, Jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM.
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), imeitaka serikali kutoa nafasi zaidi kwa Vyombo vya habari kama sehemu ya kichocheo muhimu cha kuhakikisha malengo na mipango ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 inatekelezwa kikamilifu ndani ya muda uliopangwa.
Akizungumza katika mkutano wa Wahariri na Wamiliki wa vyombo vya Habari nchini uliolenga kuhakiki Rasimu ya Taifa ya Maendeleo 2050,uliofanyika leo Disemba 16, 2024 Jijini Da es Salaam, Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile, amesema vyombo vya Habari ni kichocheo kikubwa katika kusaidia kubeba maudhui yaliyopo kwenye Dira hiyo nakuyafikisha kwa wananchi na kwamba vitumike kuhakikisha Dira 2050 inafaikiwa.
“Kwenye vichocheo tumeacha jambo la msingi sana ambalo ni vyombo vya Habari. Ile Dira ya kwanza iliviacha vyombo vya Habari, ndio mana sasa hivi tunasema tunataka tuviweke vyombo vya habari kuhifadhi utamaduni wa Mtanzania ili visaidie kubeba haya mahudhui, tuweke mpango kwamba tunapeleka utamaduni wa Tanzania” amesema Balile
Aidha Balile amezungumzia umuhimu wa ulinzi na usalama kupewa kipaumbele zaidi katika kuendana na kukabiliana na mabadiliko mbalimbali ya kidigitali yanayoshuhudiwa kote Duniani, pamoja na matumizi makubwa ya teknolojia katika suala zima la ulinzi na usalama.
Naye, Mhariri wa habari kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Anna Mwasyoke, amesema suala la kijinsia linapaswa kuangaliwa kwa jinsia zote kwani rasimu ya Dira 2050 imeainisha makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuwaacha wanaume.
Akizungumza alipokuwa akihitimisha mkutano huo, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, amesema Dira hiyo ni ya miaka ishirini na tano, lakini kutakuwa na utaratibu wa kutekelezwa katika vipindi vy miaka mitano, ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Utaratibu uliokuwepo ni kwamba ukishaandaa mpango wa mda mefu wa miaka ishirini na tano unaweza kuuweka katika mpango wa miaka mitano, mitano, lakini katika kila baada ya miaka mitano kutakuwa na uhakiki wa uteelezaji wake na kama kuna mambo yaliyojitokeza unaweza kuyaongeza“ amesema Prof. Kitila.
Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, akizungumza alipouwa akihitimisha hoja na maoni ya wahariri katika mkutano huo, uliofanyika leo Disemba 16, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa JNICC, Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO