TAARIFA KWA UMMA
Taarifa iliyo upande wa kushoto inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Jeshi la Polisi lingependa kuitolea ufafanuzi ili isiendelee kuleta taharuki ambayo si ya lazima.
Ni kweli Askari Polisi walifika eneo hilo kumkamata mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mweta, ambaye awali alikamatwa na baada ya kudhaminiwa aliruka dhamana kwa muda mrefu.
Leo Desemba 5,2024, Mlalamikaji alitoa taarifa Polisi kuwa, amemuona mtuhumiwa huyo, ikabidi askari wawahi haraka kumkamata.
Tunaendelea na uchunguzi kubaini ni nini kilichomfanya anayetajwa kwa jina la Alphonce Lusako kukimbia kisha kujirekodi video voice na kuirusha kwenye mitandao wakati siyo yeye aliyekuwa anatafutwa na Askari waliofika pale walijitambulisha kwake na kumweleza wamefika pale kwa nia ya kumtafuta Emmanuel Mweta.
Imetolewa na:
David A. Misime – DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma,Tanzania