Home BUSINESS STAMICO KUANZA USAMBAZAJI WA NISHATI SAFI YA RAFIKI BRIQUETTES ZANZIBAR

STAMICO KUANZA USAMBAZAJI WA NISHATI SAFI YA RAFIKI BRIQUETTES ZANZIBAR

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limesaini makubaiano ya mashirikiano na Usirika cha Maisha Gemu kutoka visiwani Zanzibar, ili kuwa wakala wa nishati safi na salama ya kupikia ya Rafiki Briquette visiwani humo.

Akizungumza katika hafla ya utiaji Saini hati za makubaliano iliyofanyika katika Ofisi za  STAMICO Disemba 13, 2024 Jijini  Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ushirika huo, Deusdedit Magala, amesema mashirikiano hayo yanatoa fursa kwa ushirika  wao kuwa  msambazaji wa nishati hiyo na kufanya mauzo ya moja kwa moja kwa kuanzia tani 80 hadi 100 kwa mwezi.

“Niwashukuru sana ushirika wa Maisha Gemu kwa kuibeba ajenda ya matumizi ya Nishati safi katika kutunza mazingira na kuwa vinara wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi kule Zanzibar.

“Mkataba huu unathibitisha dhamira ya makusudi ya STAMICO katika kuhakikisha mkaa huu unapatikana nchi nzima ili kushiriki kikamilifu ajenda ya Serikali ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kufikia lengo la taifa la kutunza mazigira” amesema Magala.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ushirika wa Maisha Gemu, Alawi Idarous ameshukuru hatua waliyofikia  ya utiaji sahihi mkataba huo, na kuahidi kushiriki kwa kufuata taratibu zote zilizomo katika makubaliano hayo.

Amesema uwepo wa elimu ya nishati ya Rafiki Briquettes Visiwani Zanzibar imepelekea kupatikana kwa fursa ya kibiashara, na kuhamasika kushiriki kwenye masuala ya utunzaji wa mazingira kupitia nishati hiyo.

“Mkaa huu unatarajia kuleta matokeo chanya kwa upande wa Zanzibar na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, sambamba na kutunza mazingira” amesema.

Previous articleWATENDAJI KATA NA VIJIJI SONGEA WAONYWA KUACHA UPENDELEO MCHAKATO WA KUWAPATA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII
Next articleBAADHI YA DONDOO ZA VIONGOZI WALIOZUNGUMZA KATIKA HAFLA YA UZINDUZI WA MNADA WA KWANZA WA MADINI YA VITO, MIRERANI – DESEMBA 14, 2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here