Home SPORTS SIMBA WALIPE UHARIBIFU ULIOTOKEA UWANJA WA MKAPA

SIMBA WALIPE UHARIBIFU ULIOTOKEA UWANJA WA MKAPA

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesikitishwa na vitendo vya mashabiki kung’oa na kuharibu viti vya kukalia watazamaji katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jjini Dar es Salaam katika mchezo wa kugombea Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba Sport Club ya Tanzania na Club Sportif Sfaxien ya Tunisia uliofanyika jana tarehe 15 Desemba, 2024.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Prof. Palamagamba Kabudi amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuchukua hatua mara moja kwa kuwaandikia timu ya Simba Sports Club na kuwanakili Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF) ili gharama za uharibifu uliosababishwa wakati mechi hiyo zilipwe.

Mheshimiwa Waziri Kabudi amewataka mashabiki wanaoingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuacha vitendo vya uharibifu wa uwanja kwa kuwa wanasababisha hasara kwa Serikali na kuharibu ubora wa uwanja.

“Vitendo viivyofanyika jana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa havikubariki na sio vya kimichezo, nakuelekeza Katibu Mkuu kuchukua hatua mara moja. Pamoja na kuwaandikia Simba Sports Club na TFF, wapeni ushirikiano Polisi ili watu wote waliokuwa wanang’oa viti na kuvitupa wakamatwe na wachukuliwe hatua za kisheria, lazima tabia hii ikomeshwe”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here