Home LOCAL SERIKALI IPO IMARA – MAJALIWA

SERIKALI IPO IMARA – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ipo imara na inaendelea kuwahudumia watanzania ili kuhakikisha huduma muhimu za kijami zinawafikia watanzania wote.

Amesema hayo leo (Jumamosi, Desemba 21, 2024) alipokagua alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Daraja la Sukuma linalounganisha vijiji vya Ngh’aya na Lumeji, Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza ambalo ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 10 hadi kukamilika kwake.

“Rais wetu Dkt. Samia yupo imara, katika malengo yake amedhamiria kuhakikisha kila mtanzania ananufaika kwa kupelekwa huduma muhimu kwenye maeneo yao, ujenzi wa daraja hili ni sehemu ya mikakati yake hiyo”.

Ujenzi wa Daraja hilo ambalo linaurefu wa mita 70 na barabara unganishi za Kilomita 2.3 umefikia asilimia 24 na ujenzi wake utatumia miezi 18

Mjenzi wa Daraja hilo ni mkandarasi mzawa Mumangi Construction Company ltd.

Previous articleVIDEO MPYA : KAMBI YA NYANI Ft. JULIESO – KICHWA
Next articleWAZIRI MKUU AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA MAJI KISESA, MWANZA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here