Home LOCAL RAIS SAMIA AWAAPISHA MAWAZIRI, MANAIBU NA VIONGOZI MBALIMBALI TUNGUU ZANZIBAR

RAIS SAMIA AWAAPISHA MAWAZIRI, MANAIBU NA VIONGOZI MBALIMBALI TUNGUU ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha;Mhe. Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.Mhe. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhe. Abdallah Hamis Ulega kuwa Waziri wa Ujenzi.


Mhe. Jerry William Silaa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.


Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.


Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfried Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 

Mhe. Hamis Mohamed Mwinjuma kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. James Henry Kilabuko kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) 

Mhe. Dkt. Stephen Justice Nindi, kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo (anayeshughulikia masuala ya Ushirika na Umwagiliaji), kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha mabalozi wafatao;
Bw. Anderson Gukwi Mutatembwa.

Bw. Mobhare Holmes Matinyi.
CP Hamad Khamis Hamad.
CP Suzan Salome Kaganda
Bw.Thobias Masandiko Makoba, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Mawaziri kuwatumia ipasavyo Makatibu Wakuu na wataalamu wataowakuta katika Wizara zao ili kuongeza ufanisi ndani ya Serikali katika kuwahudumia wananchi.

Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo Ikulu ndogo ya Tunguu wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, Naibu Makatibu Wakuu na Mabalozi wateule.

Aidha, Rais Dkt. Samia amesema katika kutekeleza mkakati wa taifa wa uchumi wa kidigitali ambao unachochewa na kasi ya ukuaji wa sekta ya mawasiliano na teknolojia ndani ya nchi na dunia nzima, ni vyema sasa kutenganisha majukumu hayo na yale ya sekta ya habari ili msisitizo wa kimkakati utekelezwe kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Samia amemuagiza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ashatu Kijaji kuchochea ufanisi na uimarishaji wa uchumi wa buluu pamoja na kuambatana na wataalamu katika kuwasikiliza na kutatua kero za wakulima na wafugaji.

Rais Dkt. Samia pia amemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano wa Mazingira) Mhe. Hamad Yussuf Masauni kushughulikia ipasavyo masuala ya Muungano na kumtaka kushiriki kikamilifu katika majukwaa mbalimbali ili kunapaza sauti kimataifa kuhusu masuala ya mazingira.

Vile vile, Rais Dkt. Samia amewataka Mabalozi wapya kwenda kuiwakilisha vyema Tanzania hasa katika maeneo ambayo kama taifa tuna maslahi nayo hasa zile nchi tulizoshirikiana nazo katika ukombozi wa Bara letu la Afrika. 

Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here