Home LOCAL RAIS SAMIA AOMBOLEZA KIFO CHA MWANASHERIA MKUU MSTAAFU WA SERIKALI

RAIS SAMIA AOMBOLEZA KIFO CHA MWANASHERIA MKUU MSTAAFU WA SERIKALI

Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Frederick Werema. Ninatoa pole kwa familia, Mheshimiwa Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Majaji, ndugu, jamaa na marafiki. 

Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awajalie subra na imani katika kipindi hiki cha kuomboleza msiba huu, na ailaze roho ya mpendwa wetu huyu mahali pema peponi. 

Hii ni taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyochapishwa kwenye mtandao wake wa X akiomboleza kifo cha mwanasheria Mkuu mstaafu wa Serikali marehemu Jaji Fredrick Werema. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here