Home LOCAL RAIS DK.MWINYI:ZANZIBAR IMEDHAMIRIA KUWA NA UMEME WA UHAKIKA

RAIS DK.MWINYI:ZANZIBAR IMEDHAMIRIA KUWA NA UMEME WA UHAKIKA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na wageni wake Ujumbe wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, ukiongozwa na Mhe. Rita Laranjinha (kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 7-12-2024. (Picha na Ikulu)

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na wageni wake Ujumbe wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, (kulia kwa Rais) Mhe. Rita Laranjinha na Mhe.Hans Stausboll, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 7-12-2024. (Picha na Ikulu)

ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar inadhamiria kuwa na umeme wa uhakika kutokana na kutanuka kwa shughuli za uchumi, miradi mikubwa ya maendeleo, ongozeko la hoteli za kitalii na kasi ya uwekezaji inayokuwa kila siku.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu – Zanzibar alipozungumza na Ujumbe kutoka Kamisheni ya Umoja wa Ulaya ukiongozwa na Bi. Rita Laraujinha Mkurugenzi Mwendeshaji wa masuala ya nje, Kanda ya Afrika waliomtembelea.

Rais Dk. Mwinyi ameeleza kwa muda mrefu Zanzibar imekua ikipokea megawatt 100 za umeme kutoka Tanzania Bara kupitia waya za chini ya bahari ambao kwa sasa hautoshelezi, hivyo kuna kila sababu ya kupata umeme mbadala na kufikiria kuwa na umeme wa jua, mawimbi au upepo, hivyo ameuomba Umoja wa Ulaya (EU)kuangalia uwezekano wa kuisadia Zanzibar kwenye eneo hilo.

Aidha, alisema, Serikali inafikiria kuzisarifu taka kwaajili ya kupata umeme mbadala hatua aliyoielezea mbali yakupata nishati hiyo lakini pia itadhibiditi taka kwani kumekua na changamoto kubwa ya usimamizi wa taka zinazozalishwa kila siku.

Akizungumzia uwezeshaji wanawake kiuchumi Dk. Mwinyi ameeleza nia ya Serikali kuwaongezea nguvu, uwezo na utaalamu kwa wakulima wa mwani ambao asilimia 90 ni wanawake, kwa kuliinua zao hilo pamoja na kuanzisha viwanda vidogovidogo na vya kati ili kuusarifu na kuzalisha bidhaa zinazotokana na zao hilo kwa kuziongezea thamani badala ya kuuza mwani kama malighafi.

Rais Dk. Mwinyi ameusisitiza Umoja wa Ulaya kuiungamkono Zanzibar katika azma yake ya kukuza Uchumi kupitia sekta za kimkakati ikiwemo Uchumi wa Buluu na Utalii ambazo ni Sekta za kipaumbele kwa Serikali anayoiongoza.

Amebainisha kuwa kwa sasa Zanzibar inafanya utalii wa kisasa unaoshajihisha utalii wa kumbi za mikutano, utalii michezo na wa afya ambapo awali ilijikita zaidi kuendesha utalii wa fukwe na maeneo ya urithi ambao umezoeleka kwa muda mrefu.

Akizungumzia masuala ya uwekezaji amezikaribisha nchi za Umoja wa Ulaya, hususan sekta binafsi kuja Zanzibar kubaini fursa za uwekezaji ziliopo kwani kuna maeneo mengi hayajafikiwa hasa kwa sekta ya Uchumi wa Buluu kupitia Utalii, Bandari, Mafuta na gesi pamoja na sekta ya usafirishaji wa majini. 

Pia, Dk. Mwinyi amegusia masuala ya jinsia na kueleza kuwa Serikali anayoiongoza inafanya kila juhudi kuhakikisha inaweka uwiano sawa kwa wananwake na wanaume kwa nyanja zote za Elimu, Uchumi, siasa na ustawi wa jamii na kuuomba Umoja wa Ulaya kuja kuungamkono kwenye maeneo ya taaluma, kuwajengea uwezo wanawake kwa dhamira ya kuwainua kiuchumi.

Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa ushirikiano uliopo baina yao na misaada wanayoita kwa Tanzania hususani Zanzibar kwa sekta za jamii hasa kwa Elimu, Afya na Ustawi wa Jamii na kuwaomba kuendeleza misaada hiyo.

Naye, Bi. Rita Laraujinha ameipongeza Zanzibar kwa ushirikiano wanaoutoa kwenye Miradi inayosimamiwa na EU na kumuhakikishia Rais Dk. Mwinyi kuwa wataendelea kuiunga mkono Zanzibar wa kuleta maendeleo hasa kwa masuala ya afya, elimu na Uchumi wa Buluu.

Amesema, EU imerishwa na hali ya amani na utulivu uliopo Zanzibar na kwamba Umoja huo utaendelea wakati wote kuunga mkono juhudi za kuimarisha amani hiyo na kuona Demekrasia inafuata mkondo wake kwaajili ya maendeleo ya nchi jamii kwa ujumla.

IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.

Previous articleCHADEMA KATIKA MGOGORO: VITA YA MADARAKA KATI MBOWE, LISSU
Next articleMAELFU WASHIRIKI ‘GENERATION SAMIA JOGGING’ DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here