Na. Coletha Charles, DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kuimarisha juhudi za kutunza mazingira kwa kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kuimarisha mazingira.
Amesema hayo leo tarehe 9 Desemba, 2024 kwenye makutano ya barabara ya mzungu Makutupora katika kuazimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara, wenye kaulimbiu ya Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji kwa wananchi, ni msingi wa maendeleo yetu.
Pia ameeleza kuwa kila mwananchi anawajibu wa kuchangia katika juhudi za uhifadhi wa mazingira kwa kuhakikisha wanapanda miti katika maeneo yao kulingana na uhitaji wa kuwa na Dodoma ya kijani kila mahali.
“Leo tumeanza kupanda miti katika barabara ya mzunguko. Kazi hii ni nzuri na uzuri wake ili ukamilike, tukija mwaka kesho tunaanza kuvuna maembe maana nasikia miti ya sasahivi haichelewi kubeba na hapo tutakuwa tumeona vizuri sura halisi ya mradi wa kupiganisha kijani.
Hata hivyo tunayo matumaini kupitia mradi huu Jiji la Dodoma linaenda kufanya mabadiliko makubwa katika sura yake ya ukijani wa jiji” alisema Senyamule.