Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na waumini mara baada ya kushiriki Ibada ya Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma tarehe 25 Desemba 2024.
 Â
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mapadre pamoja na waumini mbalimbali mara baada ya kushiriki Ibada ya Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma tarehe 25 Desemba 2024.
………………..Â
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Sikukuu ya Krismasi leo tarehe 25 Desemba 2024.Â
Akitoa salamu za Sikukuu ya Krismasi kupitia kwa waumini hao, Makamu wa Rais ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwatakia wakristo na wananchi wote heri ya Sikukuu ya Krismasi.
Amewasihi watanzania kusheherekea sikukuu kwa amani na utulivu pamoja na kujitoa kusaidia wale wasio na uwezo.
Makamu wa Rais ametoa wito kwa watanzania kutumia Sikukuu ya Krismasi kutafakari juu ya malezi ya watoto majumbani kwa kuwaepusha na vitendo vya ukatili wanavyopitia.
Aidha amesema ni vema kutafakari nafasi ya watoto katika Taifa kwa kuwapelekea tumaini, amani, upendo na furaha.Â
Halikadhalika, Makamu wa Rais ametoa rai kwa vyombo vya usalama kusimamia vema sheria za usalama barabarani ili Watanzania waweze kusherehekea sikukuu kwa amani.