Home LOCAL DKT. SHEIN AWATAKA WAHITIMU MZUMBE KUTOCHAGUA KAZI

DKT. SHEIN AWATAKA WAHITIMU MZUMBE KUTOCHAGUA KAZI

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM

Mkuu  wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amewataka wahitimu wa Chuo hicho kutumia maarifa waliyopata katika chuo hicho, kutengeneza fursa za ajira na kujiendeleza kimasomo nakwamba hiyo ndio njia pekee ya kufanikiwa katika maisha yao.
Amesema kuwa kusoma ni miongoni mwa njia katika kutafuta maisha nakwamba katika hilo hakuna njia ya mkato na kusisiiza kuwa  elimu haina mwisho.
Dkt. Shein aeyasema hayo katika Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, yaliyofanyika leo Disemba 5, 2024, katika Kituo Cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa mafanikio ya elimu waliyopata yana yatawawezesha kuingia kwenye ushindani wa sokola ajira hata katika mifumo isiyo rasmi ikiwemo katika Sekta Binafsi na kujiajiri wenyewe.
“Soko la ajira lina ushindani mkubwa, mjitahidi kutafuta ajira, ila kumbukeni hili mlilosikia kuwa mtu aliyehitimu chuo 1995, hakupata ajira, lakini akachagua kujiajiri Sekta ya Ufugaji, akachagua afuge kuku, kuliko kukaa bure kusubiri ajira ya serikalini na kimsingi kujiajiri kuna tija kubwa“ amesema Dkt. Shein.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Barazahicho, Profesa Saida Yahya-Othman, amewapongeza wafanyakazi wa chuo kwa kazi kubwa na adhimu wanayoendelea kuifanya ya kuwaandaa vijana, na kwamba anaamini wahitiu hao wako tayari kuikabili Dunia na changamoto zake.
“Tunaposherehekea mafanikio ya kuhitimu masomo yetu tufanye tafakuri ya maisha yetu ya chuoni na yale ya baadaye, na changamoto zitaKAzotukabili katika soko la ajira, na katika maisha yetu kwa ujumla, Changamoto ni nyingi, na zimeathiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa kiutendaji na ajira”amesema Profesa Saida.
Naye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa William Mwegoha, amesisitiza umuhimu wa kutochagua kazi badala yake kuwekeza nguvu katika  kujiajiri kwani ndio njia rafiki ya kufikia malengo.

Amewataka wahitimu  kupambana bila kuchoka pamoja na kujenga matumaini na  ujasiri pamoja na kuepuka kukata tamaa katika maisha.

Previous articleNCHI ZA EAC NA SADC ZAAZIMIA KUENDELEZA TEKNOLOJIA YA MATUMIZI BORA YA NISHATI
Next articleTRILIONI 2.9 ZA TACTIC KUBORESHA NA KUENDELEZA MIJI 45 YA TANZANIA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here