Home LOCAL DKT. MOLLEL APONGEZA JITIHADA ZA SEKTA BINAFSI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

DKT. MOLLEL APONGEZA JITIHADA ZA SEKTA BINAFSI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amepongeza juhudi na mchango wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation katika kusaidia mikakati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuboresha huduma za afya kwa watoto wenye matatizo ya mgongo wazi ili kuondoa changamoto za macho na ulemavu wa macho nchini.

Katika mazungumzo yaliyofanyika leo Desemba 14, 2024 Jijini Dar es Salama, Dkt. Mollel ameshukuru kwa msaada wa kifedha unaolenga kuimarisha jitihada hizi kwa miaka mitatu ijayo.

Aidha Dkt Mollel amemhakikishia Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Mohamed Dewji kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya chini ya Mhe. Jenista Mhagama itashirikiana naye kuhakikisha matarajio yake ya kusaidia mikakati ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inatimia.

Mo Dewji Foundation imeonesha mfano wa kuigwa kwa kuwekeza katika afya ya jamii yetu, hasa kwa makundi yenye uhitaji mkubwa kama watoto na watu wenye ulemavu wa macho.

Mazungumzo hayo yamekuwa na tija, yakiweka msingi wa ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuboresha maisha ya Watanzania kupitia huduma bora za afya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here