Home INTERNATIONAL DCEA YASHIRIKI MAFUNZO YA MTANDAO WA WANAWAKE WANAOTOA HUDUMA KWA WANAWAKE WALIOATHIRIKA...

DCEA YASHIRIKI MAFUNZO YA MTANDAO WA WANAWAKE WANAOTOA HUDUMA KWA WANAWAKE WALIOATHIRIKA NA DAWA ZA KULEVYA EGYPT

Na Prisca Libaga
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) tarehe 16 Disemba 2024  imeshiriki ufunguzi wa Mtandao wa Wanawake Wanaotoa Huduma za Tiba na Upataji Nafuu kwa Waraibu Wanawake (_Global Women Providers of Women’s Substance Use Disorders Treatment and Recovery_).
Ufunguzi wa Mtandao huo umeambatana na mafunzo ya kuwawezesha watoa huduma kupata mbinu mbalimbali za kuwaibua wanawake ambao wanatumia dawa za kulevya na kuwaunganisha pamoja na mpango wa huduma.
Mafunzo haya yatafanyika kwa muda wa siku 5 kuanzia tarehe 16 hadi 20 Disemba 2024 katika Hoteli ya Sheraton Montazah, Alexandria nchini Egypt ambapo nchi 10 za Afrika zimepata fursa ya kushiriki.
Lengo la mafunzo haya ni kuongeza uelewa kwa watoa huduma kupata mbinu za uwezeshaji kwa watoa huduma waliopo kwenye jamii ili kuibua waraibu wanawake ambao hawapo kwenye huduma na waliopo waweze kuendelea na huduma za tiba na utengamao.
Mtandao huu umezinduliwa na Prof. Menan Abdelmaksoud (_General Secretariet of Mental Health and Addiction Treatment, Ministry of Health and Population, Egypt_) ambae amesisitiza katika kuibua mbinu mbalimbali za kuwasaidia waraibu wanawake katika Nchi za Afrika.
Aidha, Mtandao huu umeandaliwa na kuratibiwa kwa ushirikiano wa  General Secretariet of Mental Health  and Addiction Treatment, Ministry of Health  and Population Egypt kwa ufadhili wa Watu wa Marekani, Drug Advisory Programme ( DAP), African Union, ISSUP, UNODC na  Colombo Plan.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here