Home LOCAL WAZAZI PONGWE WAISHUKURU JWTZ KWA MSAADA ILIYOTOA KWA WATOTO  WAO

WAZAZI PONGWE WAISHUKURU JWTZ KWA MSAADA ILIYOTOA KWA WATOTO  WAO

Wakazi wa kijiji cha Pongwe Msungura kilichoko Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani wamelishukuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa msaada mkubwa iliyoutoa kwa watoto wao.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Pongwe Msungura Bw Joel Kajonga amesema JWTZ limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi na wanafunzi wa kijijini hapo.

Naye Kamanda wa Kikosi cha 8 kinachokwenda kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Luteni Kanali Theofili Nguruwe amesema JWTZ ni jeshi la wananchi hivyo litaendelea kutoa msaada kila itakapowezekana.

Msaada uliotolewa shuleni hapo ni mahindi kwa ajili ya chakula, maharagwe, sukari, madaftari, kalamu, viatu, mabegi vyote vikilenga kuongeza morari wa kusoma kwa wanafunzi.

Mbali na msaada huo pia wataalam wa afya wa JWZT waliweza kutoa matibabu na elimu ya afya kwa wazazi wa kijiji hicho.

Previous articleWAZIRI MKUU AKAGUA MIUNDOMBINU YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI DODOMA
Next articleWAZIRI MKUU AZITAKA TAASISI ZA UMMA, BINAFSI KUACHA KUTUMIA KUNI NA MKAA KUPIKIA MWISHO MWEZI WA 12 MWAKA HUU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here