Home LOCAL WANAFUNZI SUA WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA MIONGOZO YA WIZARA YA ELIMU

WANAFUNZI SUA WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA MIONGOZO YA WIZARA YA ELIMU

 NA FARIDA MANGUBE MOROGORO

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda amewataka wanafunzi waliopata fursa ya kujiunga na chuo hicho kwa mwaka mpya wa masomo 2024/25 kufuata taratibu, sheria na miongozo iliyowekwa na Wizara ya Elimu ili kufikia malengo yao.

Amebainisha hayo wakati wa kufunga wiki ya mapokezi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza iliyofanyika katika Kampasi ya Solomon Mahlangu Mjini Morogoro ambapo amesema Menejimenti ya SUA imeaandaa miondo mbinu wezeshi ya kujifunza na kufundishia wawapo chuoni hapo.

Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii na Insia, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Samwel Kabote ambaye amemuwakilisha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala amesema SUA inamazingira mazuri ya kujifunzia ikiwemo maktaba, itakayowawezesha kusoma machapisho mbalimbali.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Mipango, Fedha na Utawala SUA Prof. Amandus Muhairwa amesema SUA itaendelea kujenga na kuboresha miundo mbinu kupitia mradi wa HEET katika Kampasi zake zote kwa kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu ili kuboresha mazingira ya kujifunzia.

Aidha, amewataka wanafunzi wote ambao ni wanufaika na mkopo wasisite kufika katika ofisi za mikopo chuoni wanapopata changamoto yoyote ya kifedha ili kupata ufumbuzi wa haraka na wenye kuepusha madhara ambayo yanaweza kuitokeza kwa wanafunzi kutotoa taarifa.

Elisa Adrea na Maliamu Juma Makoka ni wanafunzi waliojiunga na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo wameupongeza uongozi wa Chuo kwa maandalizi mazuri ya kuwapokea huku wakiwataka wanafunzi wenzao kusoma kwa bidii na kuepuka makundi yatakayowafanya kutotimiza malengo yaliyowapeleka chuoni hapo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here