Home LOCAL TRILIONI 6.7 YAFANYA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA AFYA

TRILIONI 6.7 YAFANYA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA AFYA

Na WAF – Dodoma

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema Shilingi Trilioni 6.7 zilizotolewa na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan zimechangia kuleta mageuzi makubwa ya upatikani wa huduma bora za afya ikiwemo matibabu ya kibingwa nchini.
Dkt. Mollel amesema hayo  wakati akichangia hoja kwenye Kamati ya Mipango na Uwekezaji  Novemba 07, 2024 bungeni jijini Dodoma.
“Uwekezaji wa kiasi cha Shilingi Trilioni 6.7 umeleta mabadiliko makubwa katika huduma za afya, hali ya ubora wa huduma za afya umeendelea kuimarika nchini na hospitali zote za rufaa sasa zimepata vifaa vya kisasa, ikiwemo CT Scan, huku hospitali za kanda zikifungwa mashine ya MRI, hatua inayomuweka Rais Samia katika rekodi za kihistoria,” amesema Dkt. Mollel.
Dkt. Mollel amesema kiwango cha vifo vya kina mama kimepungua kutoka 556 hadi 104, akieleza kuwa mafanikio hayo yanaonesha upunguzaji wa asilimia 81.2 katika vifo vya uzazi. 
Ameongeza kuwa Serikali imepunguza vifo vya wagonjwa wa kansa kwa asilimia 78, kutokana na upatikanaji wa matibabu ya kisasa ndani ya nchi.
Dkt. Mollel ameeleza kuwa kwa sasa Watanzania wengi hawalazimiki kwenda nje ya nchi kutibiwa, tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma  ambapo  mgonjwa aliyetakiwa kwenda India kupata matibabu alihitaji zaidi ya milioni 100, lakini sasa gharama zimepungua hadi milioni 10, huku huduma hizo zikitolewa ndani ya Tanzania. Kutokana na maboresho haya, rufaa za matibabu nje ya nchi zimepungua kwa asilimia 97.
Aidha, Naibu Waziri huyo amesema kuwa vifaa vya kisasa kama PET CT Scan vimewekwa ili kugundua kansa mapema, hata ile inayoweza kuibuka miaka 10 ijayo. Mafanikio haya yamewezesha wagonjwa 10,931 kutoka nje ya Tanzania kufika nchini kwa ajili ya matibabu, jambo linalodhihirisha uwekezaji mzuri uliofanywa na Rais Dkt. Samia katika sekta ya afya.
Previous articleSHIRIKA LA SAVE A CHILDS HEART LAIPA JKCI KIFAA CHA KUPIMA MOYO CHA TSH. MILIONI 200
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here