Home BUSINESS TCAA YAELEZA MAFANIKIO MAKUBWA SEKTA YA ANGA KWENYE MKUTANO MKUU WA 8...

TCAA YAELEZA MAFANIKIO MAKUBWA SEKTA YA ANGA KWENYE MKUTANO MKUU WA 8 WA TEF JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi amewasilisha mada kuhusu utendaji kazi wa TCAA katika Mkutano wa 8 wa mwaka wa Jukwaa la Wahiriri Tanzania (TEF),unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 06- 09, 2024 katika ukumbi wa NSSF Mafao House- Ilala.

Katika mada hiyo wahariri walipata fursa ya kuyafahamu kwa kina majukumu ya TCAA. Na pia walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali ambayo yalijibiwa na Mkurugenzi Mkuu pamoja na wataalam wa Mamlaka walioambatana naye.

Zoezi hilo la TCAA ni sehemu ya mikakati yake ya kutoa elimu kwa wadau wakuu wa vyombo vya habari inalolifanya kila mwaka.

Huu ni muendelezo wa TCAA kuutambua na kukuza ushirikiano na vyombo vya habari ambao ni wadau muhimu katika sekta ya Usafiri wa Anga nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here