Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kifaa kinachotumika kupima moyo (Transesophageal Echocardiography (TEE) probe) kwa watoto chenye thamani ya shilingi milioni 200 kilichotolewa na wataalamu wa afya kutoka Shirika la Save a Childs Heart lililopo nchini Israel wakati wa harambee ya kuchangia matibabu ya watoto iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 4.1 zilikusanywa kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto.
Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka shirika la Save a Childs Heart lililopo nchini Israel wakimfanyia mtoto upasuajiĀ wa kuziba tundu lililopo kwenye kupitia mtambo wa cathlab wakati wa kambi maalumu iliyomalizika hivi karibuni. Jumla ya watoto 19 wamefanyiwa upasuaji mdogo wa moyo.
Picha na: JKCI