Home INTERNATIONAL SAMIA SULUHU HASSAN : MWANGA WA TANZANIA KATIKA JUKWAA LA KIMATAIFA

SAMIA SULUHU HASSAN : MWANGA WA TANZANIA KATIKA JUKWAA LA KIMATAIFA

Victor Oladokun, Mshauri Mkuu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, ameielezea vyema haiba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika maoni yake ya hivi karibuni wakati wa mkutano wa G20 nchini Brazil. Akisisitiza mvuto wake, ujasiri wake, na maendeleo makubwa aliyoyafanikisha kwa Tanzania, kauli ya Oladokun inaonyesha hadhi ya Rais Samia kama kiongozi wa kimataifa.

Akiiwakilisha Tanzania kama Rais pekee mwanamke barani Afrika kwenye G20, Rais Samia anasimama imara miongoni mwa viongozi watano wa Afrika waliyoalikwa katika jukwaa hili la kimataifa. Ushiriki huu wa kipekee unaakisi ushawishi wake unaozidi kukua na kutambuliwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kimaendeleo ya Tanzania chini ya uongozi wake.

Tangu alipoingia madarakani, Rais Samia amebadilisha hali ya uchumi wa Tanzania, kushinikiza miradi ya maendeleo, na kuiongoza nchi kuelekea ukuaji usio wa kawaida. Kutoka kwa ushirikiano wa kimataifa hadi mageuzi ya ndani, uongozi wake umeifanya Tanzania kuwa mfano wa uthabiti na maendeleo duniani.

Kuhudhuria kwake mkutano wa G20 si tu hatua ya kidiplomasia; ni ishara ya maendeleo yaliyofanikishwa na serikali yake katika kuifanya Tanzania kuwa sauti muhimu katika mazungumzo ya kimataifa. Mapokezi ya joto aliyoyapata Rio yanathibitisha uwezo wake wa kuunganisha mafanikio ya ndani na matarajio ya ulimwengu.

Katika dunia ambako usawa wa kijinsia bado ni changamoto, uongozi wa Rais Samia unavunja vizuizi, ukiwahamasisha mamilioni ya wanawake na wasichana barani Afrika. Ujasiri na mvuto wake vinaukumbusha ulimwengu kwamba wanawake wanapongoza, mataifa hupiga hatua.

Wakati Tanzania ikiendelea kung’ara chini ya uongozi wake wa maono, ushiriki wa Rais Samia katika G20 ni tukio la kujivunia kwa taifa, likithibitisha dhamira yake ya kusukuma mbele matarajio ya Watanzania katika jukwaa la kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here