Home LOCAL RAIS SAMIA AONGEZA SAA 24 ZA UOKOAJI KARIAKOO

RAIS SAMIA AONGEZA SAA 24 ZA UOKOAJI KARIAKOO

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo.

Rais Dkt. Samia ametoa maelekezo hayo wakati akiongea kwa njia ya simu na Majaliwa kuhusiana na zoezi la uokoaji na kusema “Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninatambua utaratibu wa uokoaji una muda maalum wa saa 72 mpaka kusitisha zoezi hilo, binafsi nina matumaini kuwa Mwenyezi Mungu anaweza akatenda miujiza yake na kuweza kuwanusuru Ndugu zetu wengine ambao bado wamenasa kwenye jengo hilo, ninakupa maelekezo ya kutositisha zoezi la nokoaji na kuongeza muda wa saa 24 zaidi ili kuwapambania Ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hai”

Rais Dkt. Samia pia amesema “Kwa vikosi vyetu vyote na Wananchi wote wanaopambana kuokoa maisha ya Ndugu zetu katika zoezi hilo ninaomba ufikishe salamu zangu na uwaeleze kuwa natambua na ninawathamini sana, wameonesha utu, uzalendo mkubwa na uchapakazi wa hali ya juu
sana, hivyo nawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea kuwapambania Ndugu zetu kwani ninyi ni mashujaa wa Taifa letu Rais Dkt. Samia anawaombea kwa Mungu awalinde na kuwapa nguvu muda wote wakiwa wanateleleza jukumu hilo kubwa na la kizalendo”

Rais Dkt. Samia amewaombea kwa Mungu awalinde na kuwapa nguvu muda wote wakiwa wanateleleza jukumu hilo kubwa na la kizalendo na amewashi Wananchi, Ndugu na Jamaa kuendelea kuwa na subira na kama Taifa kuendelea kuwaombea Wapiganaji hao ili tufanikishe zoezi hili kwa mafanikio makubwa “Mwenyezi Mungu tunakuomba tufanyie wepesi kwenye zoezi hili,Amin”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here