Home LOCAL PEOPLE DEVELOPMENT FORUM, JENGA HUB WAZINDUA MRADI WA ‘MITANDAO SALAMA KWA WATOTO

PEOPLE DEVELOPMENT FORUM, JENGA HUB WAZINDUA MRADI WA ‘MITANDAO SALAMA KWA WATOTO

Na, Mwandishi wetu – Dar es Salaam.
Peoples Development Forum (PDF), kwa kushirikiana na Jenga Hub, imezindua Mradi wa Mitandao Salama kwa Watoto ambao utatekelezwa katika shule mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam. Mradi huu, ambao unafadhiliwa na ChildFund Korea, unalenga kulinda usalama wa watoto mtandaoni kwa kutoa elimu na kuongeza uelewa kuhusu hatari za mtandaoni na namna ya kuzibaini na kuzikabili.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Novemba 09,2024 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Miradi PDF Ramadhani Masele amesema kuwa “Watoto wanakua katika ulimwengu wa  kidijitali, ambapo fursa za mtandao ni nyingi zikiambatana na hatari nyingi zinazowakabili.
“Mradi huu unalenga kuwalinda watoto mtandaoni, kuwawezesha walimu na wazazi, na kujenga jamii yenye uelewa kuhusu usalama wa mtandaoni.” Alisema Masele
Mradi wa Mitandao Salama kwa Watoto utaendesha mafunzo na kutoa rasilimali kwa shule za msingi na sekondari, wazazi/walezi, walimu, viongozi wa serikali za mitaa, na viongozi wa dini katika wilaya zote tano za Dar es Salaam ambazo ni Ubungo, Ilala, Temeke, Kinondoni, na Kigamboni kwa Lengo la kuwapa watoto na walezi wao zana na maarifa ya kutumia mtandao kwa usalama, ili kuwawezesha watoto kuendelea kujifunza na kujiendeleza bila kuhatarisha usalama wao.
Akizungumza katika uzinduzi huo Ans. Makola kutoka dawati la Jinsia na watoto Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ameipongeza People Development Forum (PDF) na Jenga hub kwa kutoa mafunzo hayo kwa watoto na kutoa  Wito kwa wazazi, Walezi na Walimu kuchukua tahadhari na kumwelekeza mtoto jinsi ya kutumia mitandao abaki salama bila kufanyiwa ukatili kwani ni vigumu kumnyima mtoto kutumia Mtandao katika Zama hizi za Kidigitali.
“Mradi huu ni hatua muhimu ya kuwalinda watoto wetu na kuwawezesha kuelewa jinsi ya kujilinda. Tunawapongeza PDF na wadau wake kwa dhamira yenu ya kujenga mazingira salama ya mtandaoni kwa watoto wetu.” 
Ikumbukwe kuwa hatua hizi ni baada ya Serikali kupitia wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kuzindua kampeni ya ulinzi na usalama wa mtoto Mtandaoni mnamo Mnamo tarehe 11/02/2024  dhima ikiwa ni kuendelea kukabiliana na Ulimwengu wa kidigitali ili kupunguza matukio ya ukaliti mtandaoni ambayo ilienda sambamba na kauli mbiu isemayo “Ni Jukumu Letu; Chukua hatua”
Waziri wa wizara hiyo Dkt. Doroth Gwajima aliweka bayana utafiti uolifanywa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la UNICEF mwaka 2022 kuwa watoto 4 tayari ni wahanga wa ukatili huo na kuweka mikakati madhubuti ya Wizara kwa kushirikiana na wadau, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali  kumuelimisha Mtoto, kuanzishwa kwa madawati ya ulinzi na usalama wa watoto ndani na nje ya shule pamoja na kumuelimisha Mzazi juu ya matumizi sahihi ya mtandao kwa mtoto.
“Utafiti uliofanywa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la UNICEF mwaka 2022 kwa watoto wa Tanzania wa umri wa miaka 12 hadi 17 ulionesha asilimia 67 ya watoto wanatumia mitandao na asilimia 4 ya watoto hao walifanyiwa ukatili kwenye mitandao” Dkt. Gwajima.
Nao wanufaika wa Mradi huo ambao ni watoto wameahidi kufanyia kazi mafunzo waliyoyapata ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wote jinsi ya kutumia mitandao kwa manufaa hasa katika masomo yao
Previous articleBENKI YA DUNIA YAING’ARISHA TANZANIA MIRADI YA KINYWE
Next articleWAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAISLAMU WA SHIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here