Home LOCAL NIMEPIGA KURA; ILI KUTIMIZA HAKI YANGU YA KIKATIBA- MHE.KAPINGA

NIMEPIGA KURA; ILI KUTIMIZA HAKI YANGU YA KIKATIBA- MHE.KAPINGA

http://NIMEPIGA KURA; ILI KUTIMIZA HAKI YANGU YA KIKATIBA- MHE.KAPINGA

*Aungana na Wananchi kuchagua Viongozi Kitongoji cha Mheza*

*Ahimiza Watanzania kuendelea kujitokeza kupiga kura*

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga leo ameshiriki zoezi la kupiga
kura katika Kitongoji cha Mheza kijiji cha Mkumbi Halmashauri ya Mbinga Vijijini ili kuchagua viongozi wa eneo husika.

Kapinga ameeleza kuwa, kwa kufanya hivyo ametimiza haki yake ya kikatiba na kutoa wito kwa Watanzania wote kuitumia haki hiyo kikamilifu.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni miongoni mwa mihimili muhimu ya Demokrasia inayowezesha ushiriki wa wananchi katika uongozi wa maeneo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here