Home BUSINESS NHC YAPEWA TUZO YA MJENZI WA MAKAZI BORA YA UMMA YA MWAKA...

NHC YAPEWA TUZO YA MJENZI WA MAKAZI BORA YA UMMA YA MWAKA 2024 NA GLOBAL CONSTRUCTION

Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) limepewa Tuzo ya Ujenzi wa nyumba bora kwa umma na taasisi ya Dunia ya masuala ya ujenzi. Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Meneja wa Habari na Uhusiano wa NHC Bw. Muungano Saguya na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Hamis Suleiman Mwalimu, aliyemuwakilisha Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Sharif Ali Sharif.

Hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Novemba 2, 2024 ni matokeo ya kazi iliyofanywa nchini Tanzania na Kampuni ya RAFT GROUP inayojihusisha na masuala ya ukaguzi, ambayo kwa niaba ya Global Construction ilifanya utafiti, uchambuzi na uchaguzi wa kampuni mbalimbali nchini Tanzania zilizofanya vizuri katika sekta ya ujenzi ikiwemo ujenzi wa nyumba.

Hivyo, Shirika la Nyumba la Taifa likaibuka kidedea kwa kuwa kinara wa kuwezesha ujenzi wa nyumba bora za umma nchini Tanzania na kuwa na ubunifu katika sekta ya nyumba.

Previous articleMISSANA AELEZA MIKAKATI KUDHIBITI TEMBO WAHARIBIFU
Next articleJAFO AZINDUA GULIO LA BIDHAA ZA USINDIKAJI, USHONAJI NA FURSA ZA BIASHARA MKOANI LINDI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here