Home BUSINESS NAIBU WAZIRI SANGU: e-GA NI TAASISI NYETI KWA USALAMA WA NCHI 

NAIBU WAZIRI SANGU: e-GA NI TAASISI NYETI KWA USALAMA WA NCHI 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiongoza kikao kazi cha kamati yake na Watendaji wa  Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hizo 

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi , Bw. Kadari Singo,akiwasilisha hoja kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi

Mtendaji Mkuu wa e-GA, Mhandisi Benedict Ndomba,akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi 

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Hussein Amar  akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hizo 

 

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Hussein Amar  akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Taasisi ya Uongozi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hizo 

Na. Lusungu Helela

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu amesema  Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ni Taasisi nyeti kwa ajili ya  usalama  wa nchi kwani kwani hakuna Mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) uliosanifiwa unaoweza kutumika nchini katika Wizara, Taasisi  au  Idara ya Serikali bila kuridhiwa na e-GA

Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akizungumza  na Wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala   Katiba na  Sheria katika kikao cha Kamati hiyo na Watendaji wa e-GA na Taasisi ya Uongozi  kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hizo ambapo amesema  tangu kuanzishwa kwake e-GA imeleta mageuzi makubwa huku akitaja mifumo mingi inayotumika kwa sasa Serikalini imebuniwa na   kusanifiwa na e-GA

Amesema ujio wa e-GA umeisaidia kupunguza gharama kubwa kwa  Serikali ukilinganisha na hapo awali ambapo  mifumo mingi iliyokuwa ikitumika kwenye Taasisi za Serikali ilikuwa ni ya kutoka nje huku akitolea mfano mfumo  wa manunuzi  wa TANEPS ulikuwa ukimlazimisha mtumiaji endapo kama anataka kufanya marekebisho ni lazima awasiliane na watengenezaji  wa mfumo huo ambao ni  Wagiriki

”Kama nchi kulikuwa hakuna usiri wa taarifa zetu, Wasanifishaji mifumo ya TEHAMA ambao ni wa kutoka Mataifa ya nje ndo walikuwa wenye ‘serve’ za taarifa zetu  amesisitiza Mhe.Sangu

Amesema  hapo awali Taasisi nyingi za Serikali zilikuwa zikitumia mifumo hiyo ya kutoka nje bila kuidhinishwa na e-GA ambapo ilikuwa  ni rahisi kuhujumu kwa lengo la kujinufaisha kwa kushirikiana na watu wa kutoka  nje ila kwa sasa hilo jambo haliwezekani kutokana na uwepo wa e-GA 

‘”Upo ushahidi kabisa kwamba e-GA imesaidia kuboresha utendaji kazi, imeimarisha utawala bora, kupunguza vitendo vya rushwa ambavyo vingeweza kujitokeza, kuimarisha makusanyo na kudhibiti matumizi ya maduhuli ya serikali” Mhe. Sangu amesisitiza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala,  Katiba na  Sheria  Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ameipongeza e-GA kwa kazi kubwa inayoendelea kuifanya huku akiitaka kjiimarisha zaidi kwenye eneo la ubunifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia yanayotokea dunia kote

Hata hivyo Mwenyekiti huyo ameitaka e-GA kusanifu mifumo itakayosaidia kupunguza matatizo katika jamii ikiwemo upotevu mkubwa wa maji unaotokea  katika maeneo mbalimbali nchini.

Previous articleMSIMMU WA SITA GOBA HILLS MARATHON KUFANYIKA FEBRUARI 1-2024
Next articleDC NASSARI AFUNGUA KONGAMANO LA WAFANYABIASHARA WILAYANI MAGU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here