Home LOCAL MAANA YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUIFUNGUA NCHI.

MAANA YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUIFUNGUA NCHI.

Tangu aingie madarakani Machi 2021 hadi Agosti 2024, Rais Samia Suluhu Hassan ameufungua uchumi wa Tanzania kwa dunia na kujenga mazingira bora ya biashara za kimataifa.

Matokeo ya juhudi hizi yanaonekana wazi katika ukuaji wa biashara yetu kimataifa, kutoka USD 17.4 bilioni (Mauzo nje – $8.4bn, Uingizaji bidhaa – $9bn) hadi kufikia USD 31.4 bilioni (Mauzo nje – $15bn, Uingizaji bidhaa – $16.4bn). Hii ni sawa na ongezeko kubwa la 84%!

Huku tukishuhudia ongezeko hili la kibiashara, deni la nje limeongezeka kwa asilimia 33%, kutoka $24.4 bilioni hadi $32.6 bilioni, ambalo ni jambo la kawaida kwa nchi zinazopiga hatua za kimaendeleo kupitia uwekezaji wa kimkakati.

Kwa kufanya hivyo, Rais Samia amefungua milango ya fursa mpya kwa Watanzania na kukuza uchumi kwa kuhakikisha Tanzania inakuwa sehemu ya ushindani wa kibiashara duniani.

Twende pamoja na Mama kwa maendeleo zaidi!

Chanzo benki kuu ya Tanzania monthly Economic Review May2021 and Monthly Economic Review for October 2024

Previous articleMBINU MPYA YA KUWADHIBITI TEMBO YAONESHA MWELEKEO WA MAFANIKIO SAME
Next articleSERIKALI, NMB KUSHIRIKIANA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here