Home LOCAL LEMA AMTUHUMU KIGAILA KUSABABISHA VURUGU ZA CHADEMA ARUSHA

LEMA AMTUHUMU KIGAILA KUSABABISHA VURUGU ZA CHADEMA ARUSHA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amedai vurugu zilizojitokeza juzi wakati wa uchaguzi wa kutafuta viongozi wa chama Mkoa wa Arusha zilichochewa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Benson Kigaila..

Lema ameyabainisha hayo leo Novemba 16,2024 wakati akizungumza na wanahabari jijini Arusha.

“Hii ilikuwa ni organised crime kati ya watu wa CHADEMA na ndiyo maana na ninyi waandishi wa habari mlipatikana.Cha kusikitisha zaidi na hii ninaogopa kusema kwa sababu ninalisema, lakini ninaumia sana.

“Cha kusikitisha zaidi yale mambo mimi nilimuomba Naibu Katibu Mkuu Bara ateremke,Bw.Benson Kigaila…ateremke na nilimuomba ateremke awazuie wale wafanya fujo kwa sababu mmoja wa wafanya fujo ni rafiki yake mkubwa.

“Ambaye siku chache zilizopita alifanya fujo Monduli, mmoja wa wafanya fujo na alipofanya fujo Monduli mpaka uchaguzi wakamtukana msimamizi.

“Halafu wakati wakifanya fujo Monduli, mimi nilishuhudia kwamba, msimamizi alinipigia simu, nikamwabia afadhali hapa nipo na msimamizi wa uchaguzi Bw.Benson Kigaila unaweza ukaongea naye akasema hawa wanataka kunipiga.

“Wamepora na matokeo ya mabaraza,sasa sijui waliongea nini, lakini alisema kama uchaguzi wa wilaya haujatimia funga, halafu watu wa hamasa wakuondoe hapo muondoke.

“Kesho yake, mimi nikiwa na Benson Kigaila mmoja wa wafanya fujo akampigia simu, akaongea nae kama dakika 20.

“Niko na Benson, Moshi nikamwambia Benson, Naibu Katibu Mkuu Bara hawa watu wamefanya fujo, wamedhalilisha watu.

“Unapowapa audience ya kuongea nao na unapokuwa submissive kwao, alikuwa akiongea naye yeye akionekana kuwa mnyenyekevu kwao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here