Home LOCAL KADA WA CCM ALEX MSAMA AWAOMBA WATANZANIA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA

KADA WA CCM ALEX MSAMA AWAOMBA WATANZANIA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA

Kada wa Chama cha mapinduzi CCM, Alex Mwita Msama ambaye pia ni Mkurugenzi wa Dira TV Tanzania amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuwachagua viongozi mbalimbali wa Serikali za mitaa siku ya kesho tarehe 27 Novemba 2024 .

Ndg Alex Msama amesisitiza kuwa viongozi wa Serikali za mtaa wamekuwa muhimili mkubwa sana na chachu ya maendelea kwa ngazi za Mitaa,

“Niwaombe watanzania wote kesho tujitokeze kwa wingi kupiga kura kuchagua viongozi wetu wa Serikali za mitaa kwa maendelea ya wananchi na mitaa yetu” Alex Msama

Uchaguzi wa Serikali za mitaa utafanyika siku ya kesho tarehe 27 Novemba Tanzania nzima ambapo wananchi watapata nafasi ya kuchagua viongozi wao wa serikali za mitaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here