Home LOCAL Dkt. NDUGULILE AFARIKI DUNIA

Dkt. NDUGULILE AFARIKI DUNIA

Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson kwa masikitiko makubwa ametangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia leo November 27, 2024 Nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Dkt. Tulia amesema “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa Familia, Wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote, Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi”

“Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa, Bwana ametoa na Bwana ametwaa, apumzike kwa amani

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here