Home BUSINESS BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA YAFIKIA DOLA BIL. 8.78-MAJALIWA

BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA YAFIKIA DOLA BIL. 8.78-MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla ya Kumbukumbu ya Miaka Kumi ya Jumuiya ya kukuza Ushirikiano kati ya China na Tanzania iliyofanyika kwenye ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kiki cha Dar es salaam, November 30, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*_Asema Rais Dkt. Samia anathamini mchango wa China kwenye maendeleo nchini_*

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na China umeendelea kukua ambapo mwaka 2023 biashara kati ya nchi hizo ilifikia dola bilioni 8.78.

Amesema kuwa ukuaji na ushirikiano huo wa makampuni ya China na wafanyabiashara wa Tanzania umeleta maendeleo katika ukuaji wa viwanda vya ndani, kutengeneza ajira, ujenzi wa miundombinu na uboreshaji wa hali ya maisha ya Watanzania.

Amesema hayo leo (Novemba 30, 2024) wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Miaka Kumi ya Jumuiya ya Kukuza Ushirikiano kati ya China na Tanzania, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Dar ea Salaam, Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Kampuni za China zimezindua takribani miradi 1,274 ambayo kwa kiasi kikubwa pamoja na mambo mengine, imezalisha ajira kwa Watanzania. “Huu ni uthibitisho wa jinsi ushirikiano wetu unavyolenga kutoa fursa kwa wananchi wetu”.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anathamini mchango wa China katika maendeleo ya Tanzania kwenye sekta mbalimbali zikiwemo za biashara, miundombinu na utamaduni”

Aidha amesema kuwa China ni moja ya mshirika mkubwa wa kibiashara na uwekezaji kwa Tanzania na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo kwenye sekta za kilimo, madini, viwanda na maendeleo ya miundombinu.

Ameongeza kuwa China imekuwa mshirika muhimu katika kuisaidia Tanzania kukabiliana na majanga ya kiafya ikiwemo magonjwa ya kuambukiza na changamoto za afya ya mama na mtoto. “China imekuwa ikitoa timu za wataalam, kuchangia vifaa, na kusaidia kujenga miundombinu ya afya. Ushirikiano huu umeokoa maisha ya wengi na umehakikisha kwamba watu wetu wanapata huduma bora za matibabu”

akizungumza kuhusu Jumuiya ya Kukuza Urafiki kati ya Tanzania na China, Mheshimiwa Majaliwa amesema jumuiya hiyo imekuwa mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ikiwemo kuwaleta watu pamoja, si tu kutoka kwa serikali, bali kutoka nyanja mbalimbali za maisha.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Jumuiya  ya Kukuza Ushirikiano Kati ya Tanzania na China, Mizengo Pinda alipowasili kwenye  ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuwa mgeni rasmi katika hafla ya Kumbukumbu ya Miaka Kumi ya Jumuiya ya Kukuza Ushirikisao kati ya China na Tanzania, November 30, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vito alipotemblea banda la manesho  la  kampani ya TANSO  katika  hafla ya Kumbukumbu ya Miaka Kumi ya Jumuiya ya kukuza Ushirikiano kati ya China na Tanzania iliyofanyika kwenye ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, November 30, 2024. Kulia ni Afisa wa kampuni hiyo, Allen Su.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, viongozi na waalikwa wakitazama video  katika hafla ya Kumbukumbu ya Miaka Kumi ya Jumuiya ya kukuza Ushirikiano kati ya China na Tanzania iliyofanyika kwenye ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kiki cha Dar es salaam, November 30, 2024. Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini, Chen Mingjian na kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla ya Kumbukumbu ya Miaka Kumi ya Jumuiya ya kukuza Ushirikiano kati ya China na Tanzania iliyofanyika kwenye ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kiki cha Dar es salaam, November 30, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here