Home BUSINESS WAZIRI JAFO AMUWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA COMESA NCHINI BURUNDI

WAZIRI JAFO AMUWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA COMESA NCHINI BURUNDI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani S. Jafo leo tarehe 31 Oktoba 2024 amemuwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Soko
Huru la Kusina na mashariki mwa Africa(COMESA).

Mkutano huo umefanyika katika Jiji la Bujumbura nchini Burundi ukilenga kuimarisha Mtengamano wa kikanda kupitia kuongeza thamani kwa kilimo himilivu kwa mabadiliko ya Tabianchi na thamani ya Madini,na kuimarisha Utalii.

Tanzania inashiriki mkutano huo kama waangalizi kwani Tanzania bado ipo katika
Mchakato wa kikamilisha utatu wa EAC-SADC-COMESA.

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo ni moja na kuongeza fursa ya nchi ya Tanzania katika masuala ya biashara na kujenga uchumi wa nchi.

Previous articleWADAU WA MAENDELEO TUSHIRIKIANE UTEKELEZAJI WA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE” – MAJALIWA
Next articleBoT YATANGAZA UKOMO MATUMIZI NOTI ZA ZAMANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here