Home LOCAL WANAHARAKATI WANAOMCHAFUA RAIS SAMIA WAUMBUKA  

WANAHARAKATI WANAOMCHAFUA RAIS SAMIA WAUMBUKA  

Taasisi moja inayo husishwa na baadhi ya wanaharakati waliojificha Nairobi inadai CCM Tanzania imenunua haya magari kwa bei ya $200,000 (TZS 540,000).

Uki-search Google kwa haraka haraka tu, utagundua picha zilizo postiwa kwenye ukurasa wa taasisi hiyo zinatoka kwenye makala ya BBC Top Gear yenye kichaa cha habari “This Secret Dealer Is Selling New Old Toyota Land Cruisers That Are Supposed To Save The World.” 

Picha hiyo inayo daiwa na taasisi hiyo kuwa imepigwa picha kwenye eneo la chini la kuegesha magari ya UVCCM pale Lumumba kiuhalisia ni picha ya Toyota 650 ambazo zipo kwenye stoo moja nchini Uholanzi zikisubiria wateja.

Genge hili limekuwa likimchafua Mhe. Rais kwa mambo ya uongo na uzushi pamoja na familia yake na watu wake wa karibu, Tulijua genge hilo limeishiwa hoja kwa muda mrefu ila hatukujua wameishiwa kiasi hichi. Sasa hivi wanaishia kutunga hadithi kila leo ambazo hazina ukweli kwa lengo la kuendeleza ajenda zao.

Ila hatushangai. Tunajua bila ajenda hizi Mwanaharakati huyo anayeishi Nairobi atakosa hela za wafadhili na hela za kuwalipa posho vijana wake amaowatumia kusambaza ajenda zake.

Ni wakati sasa Mwanaharakati huyu atumie kipaji chake cha kutengeneza uongo aanze kutunga script za tamthilia ili alipwe kuweka hadithi zake kwenye luninga. Hakika Mwanaharakati huyu ni director wa uongo na Mariawood ndio kiwanda cha kutengeneza uongo huo. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here