Home BUSINESS TPA YAPONGEZWA KWA MCHANGO WAKE KATIKA ZEKTA YA MADINI

TPA YAPONGEZWA KWA MCHANGO WAKE KATIKA ZEKTA YA MADINI

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepongezwa kwa mchango wake katika maendeleo ya Sekta ya Madini pamoja na Sekta nyingine Nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa alipotembelea Banda la TPA katika maonesho ya Saba ya Teknolojia na Madini yanayoendelea Mkoani Geita.

Mhe. Naibu Waziri Kiruswa amesema, TPA ni Mdau muhimu katika hatua zote za mnyororo wa thamani wa Sekta ya madini na kupongeza huduma nzuri za TPA kwa Wadau wa Sekta ya madini akitolea mfano kuongezeka kwa ufanisi wa huduma kipindi hiki ambapo Serikali na inashirikiana na Wabia kutoa huduma katika Bandari ya Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here