Home BUSINESS TANZANIA INAVYOONGOZA KATIKA KUPAMBANA NA UMASKINI AFRIKA

TANZANIA INAVYOONGOZA KATIKA KUPAMBANA NA UMASKINI AFRIKA

 

Tunapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umaskini (Oktoba 17), Tanzania inajitokeza kuwa kielelezo cha matumaini na maendeleo.
Kwa mujibu wa takwimu za Afrobarometer, asilimia 51 ya Watanzania wanaamini kuwa serikali yao inafanya kazi nzuri au nzuri sana katika kuwaondoa watu kwenye umaskini, na kuiweka Tanzania kuwa miongoni mwa nchi mbili pekee za Afrika ambapo idadi kubwa ya raia wana imani na juhudi za serikali yao – ya pili kwa Zambia (asilimia 54).

Hii ni ishara ya mafanikio ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kupambana na umaskini na kuboresha hali za maisha ya mamilioni ya Watanzania.
Wakati serikali nyingi za Afrika zinakabiliwa na changamoto za kukidhi matarajio ya raia wao, Tanzania inabaki mstari wa mbele, ikionyesha kuwa kwa uamuzi thabiti, uongozi imara, na sera madhubuti, maendeleo yanawezekana.
Tuendelee kushirikiana kujenga Tanzania yenye ustawi na isiyo na umaskini kwa wote!

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here