Home LOCAL TAMASHA LA 43 LA BAGAMOYO KUITANGAZA NCHI KIMATAIFA

TAMASHA LA 43 LA BAGAMOYO KUITANGAZA NCHI KIMATAIFA

Wafanyabiashara na wajasiriamali wa sanaa za ufundi wanatarajiwa kunufaika na Tamasha la 43 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku Nne Mfululizo katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Mkoani Pwani kuanzia Oktoba 23 hadi 26, 2024.

Akizungumza na waandishi wa Habari Bagamoyo Mkoani Pwani Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa lengo la Tamasha halitakuwa ni Kuitangaza Bagamoyo pekee bali Nchi nzima na Afrika Mashariki.

Amesema Wafanyabishara hao wataweza kuonesha na kuuza bidhaa zao kitaifa na kimataifa ikiwemo Batiki, Shanga Magauni, Hereni, vikapu Ngoma, picha Michoro ,Mashati, Virutubisho na Tibalishe.

Tamasha hilo ambalo litazinduliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro linalenga kuvutia Wadau wa Nje na Ndani ya Nchi ambapo pia litahusha shughuli za kisanii, Kiutalii, kijamii na Kiuchumi.

Pia, Amesisitiza Maandalizi ni mazuri na tayari kwa ajili ya kupokea wageni kutoka Mataifa mbalimbali Duniani huku burudani bora zaidi zikitarajiwa kulinganisha matamasha mengine yaliyowahi kufanyika.

Aidha, Mhe Mwinjuma Amesema kuwa Lengo la sasa ni kuhakikisha wanafikia Tamasha la siku saba tofauti na ilivyo sasa la siku nne ili kusaidia vivutio vyote vya Utalii vilivyopo bagamoyo vinajulikana Dunia nzima

Naye Mkuu wa Taasisi ya Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye ameeleza Kuwa Tamasha hilo linatarajiwa kuhudhiriwa na Viongizi wa serikali, Makampuni Binafsi, Vyama vya siasa na Viongozi wa Dini mbalimbali.

Dkt. Makoye amesema pia Tamsha hili litahusisha Vikundi 74 ambapo vikundi 61 ni kutoka Tanzania Bara, 2 kutoka Zanzibar na 11 vya kimataifa kutoka Afrika Kusini Zambia, India, Ujerumani, Brazili Hispania, Botswana, na Visiwa vya Mayotem (Ufaransa).

Vikundi hivyo vitafanya maonesho Jukwani ikiwemo Ngoma za Asili, Mziki wa Asili na wa kisasa Maigizo, Sarakasi, Vichekesho na Mazingaombwe.

Aidha, Tamasha hili litatangiliwa na Mkesha maalumu utakaofanywa usiku wa leo jumanne tarehe 22 kuamkia jumatano ya tarehe 23 Oktoba 2024.

Previous articleKAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA UTENDAJI KAZI WIZARA YA NISHATI
Next articleDKT. MWAMBA AJADILI UFADHILI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here