Home BUSINESS SERIKALI YASEMA UBIA WA BARRICK NA TWIGA UNAZIDI KULETA MANUFAA NCHINI

SERIKALI YASEMA UBIA WA BARRICK NA TWIGA UNAZIDI KULETA MANUFAA NCHINI

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa
 
*Ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania iliyotolewa hivi karibuni imebainisha hakuna ukiukaji wa haki za Binadamu North Mara.
 
***
 
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema  ubia kati ya Kampuni ya Dhahabu ya Barrick na Serikali ya Tanzania unazidi kuleta manufaa nchini na  kwamba serikali itaendelea kuwalinda wawekezaji wenye kuleta mapinduzi chanya katika kukuza uchumi wa nchi.
 
Akiongea na katika mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali uliofanyika leo Jumamosi Oktoba 5,2024 katika ukumbi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu ,Dkt. Kiruswa amesema Serikali haitafumbia macho vitendo vya kuwahujumu wawekezaji wanaofanya vizuri katika uwekezaji wao kwa lengo la kuwakatisha tamaa na kurudisha nyuma mkakati wa Serikali wa kukuza uwekezaji nchini zikiwemo taasisi za nje zinazodai zinatetea haki za Binadamu ambazo zimekuwa zikijifanya zinatetea watanzania wakati zinatafuta mianya ya kujinufaisha kupitia mgongo wa watanzania kwa kuibua madai ya uongo dhidi ya wawekezaji wakati Serikali inavyo vyombo na taasisi thabiti za kuhakikisha wawekezaji wanafuata kanuni na sheria za nchi.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa.
 
 Dkt. Kiruswa amesema kuwa kwa  kipindi kirefu kumekuwepo na ombi la wadau mbàlimbali kutaka makampuni makubwa ya uchimbaji kusaidia wachimbaji wadogo suala alilodai limeanza kufanyiwa kazi.
 
Ubia kati ya Kampuni ya Dhahabu ya Barrick na Serikali ya Tanzania unachangia 51% ya mapato ya Serikali yanayotokana na tasnia ya uchimbaji madini, kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Mpango wa Uwazi wa Tasnia ya Uchimbaji Madini Tanzania (TEITI). Ubia wa Twiga unajumuisha migodi ya dhahabu ya North Mara na Bulyanhulu.
 
Migodi yote miwili pia iliongoza katika utendaji wa kiusalama wa tasnia hiyo, huku Bulyanhulu ikishinda Tuzo ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka huu wakati North Mara ikitajwa na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya Tanzania (OSHA) kuwa kampuni bora katika kuwahudumia wafanyakazi wenye mahitaji maalumu.
 
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, amesema katika mkutano huo kuwa utafutaji wa madini unaoendelea katika maeneo yaliyotumika na kuachwa karibu na migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara unaendelea. 
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow.
 
Amesema Utafiti huo umebainisha fursa zaidi za kuzihuisha na kuzipanua hifadhi za madini ambapo madini yatakwisha au kupungua, jambo litakalosaidia zaidi katika kuongeza uhai na unyumbufu wa migodi hiyo.
 
 Aidha, maendeleo mazuri yameshapatikana katika kuyabainisha maeneo mapya ambapo hapakuwahi kuwa na shughuli za uchimbaji madini, yenye uwezo wa kuongeza migodi mipya kwenye kampuni hiyo.
 
Bristow amesema mpango wa Barrick na Twiga wa Kusongesha Mbele Mustakabali wa Elimu umekamilisha awamu yake ya kwanza, ambapo Barrick ilifadhili upanuzi wa miundombinu ya shule zipatazo 64, yenye thamani ya dola milioni 10, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa vipatavyo 396, mabweni yapatayo 97 na majengo ya maliwato yapatayo 600. Awamu ya pili ya mpango huo umepangwa kuanza katika robo ya nne ya mwaka huu kwa uwekezaji mwingine wa dola milioni 10 ambao utafuatiwa na awamu ya tatu ya dola milioni 10.
 
Wakati huohuo, Chuo cha Barrick, kilichozinduliwa mwanzoni mwa mwaka na Waziri wa Madini kwenye mgodi uliofungwa wa Buzwagi na ambao hivi sasa ni eneo maalum la uzalishaji (SEZ), tayari kimetoa mafunzo kwa mafomeni, wasimamizi na warakibu zaidi ya 1,000 kutoka katika nchi za Afrika na Mashariki ya Kati. Chuo hiki kiko mbioni kufikia lengo lake la kutoa mafunzo kwa zaidi ya watu 2,000 mwaka huu.
 
Bristow amesema kulingana na dhamira ya uwazi ya Barrick, kampuni hiyo iliwasilisha taarifa za hivi karibuni za mfululizo wa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu zilizokuwa zinatolewa dhidi ya Mgodi wa North Mara kwenye Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania (CHRGG). Baada ya kutembelea mgodi huo na maeneo ya jirani na kufanya uchunguzi wa kina, tume hiyo ilitoa taarifa iliyothibitisha kwamba hapakuwa na ushahidi wa ukiukwaji wa haki za binadamu katika mgodi wa North Mara na hivyo kuuondolea mgodi huo tuhuma hizo zilizotolewa na baadhi ya mashirika yasiyo yasiyo ya kiserikali ya nchi za nje.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali uliofanyika Jumamosi Oktoba 5,2024  – Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.

Meneja wa Barrick nchini  Melkiory Ngido akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.

Meneja wa Barrick nchini Melkiory Ngido kizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.
Meneja wa Barrick nchini Melkiory Ngido akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akiteta jambo na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa (kushoto).
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akiteta jambo na Meneja wa Barrick nchini Melkiory Ngido (kulia)
Mkutano ukiendelea
Mkutano ukiendelea

Meneja wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Victor Lule akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mhe. Grace Kingarame akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza  kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.
Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale, Mhe. Hussein Nassor Amar (Kassu) akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.
Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Iddy Kassim akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kupokea taarifa ya utendaji wa migodi ya Barrick uliojumuisha wadau mbalimbali.
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa mkutano huo
Wafanyakazi wa Barrick wakifuatilia matukio wakati wa mkutano huo
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa mkutano huo
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa mkutano huo
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa mkutano huo
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa mkutano huo
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa mkutano huo
 
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here