Home BUSINESS RAIS SAMIA AZINDUA TUME YA MABORESHO YA KODI IKULU

RAIS SAMIA AZINDUA TUME YA MABORESHO YA KODI IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Oktoba, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Oktoba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi mara baada ya hafla ya uzinduzi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Oktoba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ili kufikia lengo la kujenga uchumi jumuishi, unaokua kwa kasi, unaoimarisha ustawi wa watu kwa kuboresha huduma za jamii na kupunguza umaskini wa kipato kwa mtu mmojammoja, nchi inapaswa kuwa na mfumo mzuri wa ulipaji na ukusanyaji wa kodi.  

Rais Dkt. Samia amesema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Rais ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi iliyofanyika Ikulu. 

Aidha, Rais Dkt. Samia amesema kwa kuzingatia mrejesho na maoni mbalimbali ya wananchi, wadau wa sekta binafsi na wawekezaji wengine, Tume hiyo imeundwa kwa lengo la kufanya tathmini ya mfumo mzima wa kodi, kuimarisha zaidi mfumo huo na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kurahisisha usimamizi wa ukusanyaji wa kodi nchini.

Rais Dkt. Samia amebainisha kuwa licha ya uchumi wa nchi kukua kwa kasi, idadi ya watu kuongezeka na mahitaji ya huduma za jamii na miundombinu kukua, bado asilimia 60 ya uchumi wa nchi unatokana na sekta isiyo rasmi. 

Rais Dkt. Samia amesema Serikali  imedhamiria kujenga  mfumo wa kodi unaotenda haki, ambao utamuwezesha kila anayestahili kulipa kodi kulipa kodi stahiki na kutoza kodi zote kwa mujibu wa sheria. 

Pia amesisitiza umuhimu wa nchi kuwa na mfumo wa kodi unaochochea ukuaji wa uchumi wa viwanda na kuchangia ujenzi wa uchumi jumuishi, unaoiwezesha Serikali kuwa na vyanzo vya uhakika na vinavyotabirika ili kuleta ustawi kwa wananchi. 

Aidha, Rais Dkt Samia ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuiwezesha nchi kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa mwezi Septemba 2024. Amesema hatua hiyo umechangiwa na jitihada za Serikali kuimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato, kuijengea uwezo TRA, na kuimarisha mazingira ya kufanyia biashara nchini ikiwemo kufuta baadhi ya tozo na kuimarisha utendaji kwenye Idara, Wakala na Taasisi za Serikali.

Jitihada hizo zimeendelea kuleta matokeo chanya ya kuongezeka kwa makusanyo ya kodi na kuongeza ulipaji kodi kwa hiari.

Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Previous articleTCU YAONGEZA MUDA WA UDAHILI WANAFUNZI ELIMU YA JUU
Next articleTANZANIA YAJIPANGA KUTUMIA NISHATI YA NYUKLIA KUZALISHA UMEME
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here