Mnada wa kwanza wa korosho kwa msimu wa 2024-2025 umefanyika kupitia chama kikuu cha ushirika cha TANECU kinachohudumia wilaya ya Tandahimba na Newala mkoani Mtwara.
Jumla ya tani 3,857 za korosho ghafi ziliuzwa kwa kutumia mfumo wa soko la bidhaa Tanzania (TMX) Bei ya juu iliyofikiwa ni shilingi 4120 kwa kilo na bei ya chini ni shilingi 4,035 kwa kilo kutoka bei ya shilingi 2500 kwa kilo.
Wakulima wa kutoka Tandahimba na Newala wanaishukuru serikali ya Rais Samia kwa kusikia kilio chao kwa bei nzuri ambayo haijawahi kutokea kwani kwa miaka kadhaa nyuma bei haikuwa nzurii.