Home LOCAL RAIS SAMIA AKIWA PAMOJA NA WENZA WA VIONGOZI KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI

RAIS SAMIA AKIWA PAMOJA NA WENZA WA VIONGOZI KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya Wenza wa Wakuu wa nchi mbalimbali Barani Afrika kabla ya kufungua Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba, 2024.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba, 2024. Mkutano huo unahudhuriwa na watu kutoka nchi mbalimbali, ambapo miongoni mwao ni Wenza wa Wakuu wa Nchi 15 za Afrika na Asia, Watunga Sera, Wanataaluma, Watafiti na Wanahabari wa masuala ya Afya kutoka nchi mbalimbali duniani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here